HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MBUNGE LUCY OWENYA AWAFARIJI WAATHIRIKA WA MVUA ILIYOSABABISHA MAFURIKO MOSHI VIJIJINI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mafuriko makubwa yamevikumba vijiji saba kikiwemo kiwanda cha sukari cha TPC na kuathiri miundombinu pamoja na makazi ya watu kujaa maji.
Kutokana na hali hiyo Mbunge Lucy Owenya alilazimika kutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akimfariji mmoja ya waathirika wa mafuriko hayo aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya kupoteza vitu vyake mbali,mbali ikiwemo vyeti vya taaluma ya utabibu.

Mifugo pia liathirika na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akikabidhi msaada wa chakula kwa wananchi walioathirika na mafuriko hayo.
Mbunge wa viti maalumu ,Lucy Owenya (Chadema) (kulia)akiwa ameongozana na diwani wa kata ya Arusha Chini ,Rojas Mmari alipotembelea kujionea athari zilizotokana na mafuriko hayo.
Mbunge Lucy Owenya akitembelea maeneo yaliyo athirika na mafuriko hayo.
Eneo lililobomolewa ili kuruhusu maji ya mafuriko kupita.
Baadhi ya nyumba zilijaa maji hali iliyowalazimu wahusika kutoa itu vya ndani nje.
Wengine walilazimika kuweka vyakula juu ya mabanda ya kuku.
Baada ya maji kujaa wengine walilazimika kuhamishia magodoro yao juu ya paa la Choo.
Hata vyakula ambavyo vingi vyao vililowa na maji vilianikwa juu ya paa.
Mbunge Lucy Owenya akitizama namna ambavyo baadhi ya wananchi walivyoamua kuokoa vitu ya kwa kuianika juu ya paa.
Mbunge Lucy Owenya akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo.
Diwani wa kata ya Arusha Chini Rojas Mmari akizungumza jambo mara baada ya wananchi wake kukabidhiwa msaada huo.
Afisa mtendaji Utawala wa kiwanda cha sukari cha TPC ,Jafary Ally akizungumza kuhusu namna mafuriko hayo yalivyo athiri kiwanda hicho.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: