Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Bondia wa Marekani Floyd Mayweather ameshinda pigano lililosubiriwa kwa hamu na na watu wengi ulimwenguni kote. Bondia Floyd Mayweather ameshinda mchezo huo kwa point 118-110, 116-112, 116-112 kutoka kwa waamuzi wa mchezo huo na kunyakuwa mkanda wa WBC huku akiifanya rekodi yake ya kutopigwa kufikia michezo 48.


Bondia huyo ambaye hajashindwa alimshinda mpinzani wake raia wa Ufilipino Manny Pacquiao kwa wingi wa pointi.

Pambano hili la kihistoria na lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na watu wengi Duniani, liliopigwa leo asubuhi kwa muda wa Afrika ya Mashariki kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa MGM Grand Garden Arena, jijini Las Vegas, Marekani.
ENDELEA KUTAZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Mchezo ulikuwa ni mkali sana na Mabondia wote walikuwa wakirushiana makonde kwa zamu.

Mashabiki wengi waliojaa katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini Las Vegas walimzoma mara kwa mara Mayweather.

Kote duniani wateja millioni 3 walilipa kuliona pigano hilo ambalo ndio pigano lililovutia kitita kikubwa cha fedha katika historia ya ndondi.

Bondia Floyd Mayweather akimsikiliza baba yake wakati wa mapumziko

Tiketi nyingi za pigano hilo ziliuzwa katika bei ya makumi ya maelfu ya dola.





Mechi ikiendelea

Referee wa mchezo huo Kenny Bayless akiendelea kuchezesha pambano hilo lililopigwa leo asubuhi kwa muda wa Afrika ya Mashariki kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa MGM Grand Garden Arena, jijini Las Vegas, Marekani

Bondia Floyd Mayweather akishangilia ushindi wake baada ya kumchapa mpizani wake aia wa Ufilipino Manny Pacquiao.

Manny Pacquiao akiwa katika hali ya sintofahamu baada ya pambano kuisha



Mabondia Manny Pacquiao(kulia) na Floyd Mayweather(kushoto) wakifurahi pamoja mara baada ya mpambano lao kuisha

Bondia Floyd Mayweather akishangilia mara baada ya pambano kuisha


Bondia Floyd Mayweather Jr akiwa na mikanda yake na tuzo aliyoshinda katika michezo mbali mbali



No comments:
Post a Comment