Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, kushoto, akizungumza jambo baada ya kutangaza kusogeza mbele huduma ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ambapo sasa huduma hiyo imepelekwa mbele hadi Juni 30, mwaka huu. Picha na Mpiga Picha wetu.
Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kulia akizungumza jambo baada ya kutangaza kusogeza mbele huduma ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ambapo sasa huduma hiyo imepelekwa mbele hadi Juni 30, mwaka huu. Picha na Mpiga Picha wetu.
TAASISI
ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya
mikopo imesogeza mbele huduma yao mpya ya mikopo ya viwanja vilivyopo
Vikukuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa ajili ya kutoa fursa zaidi
ya Watanzania kupata viwanja hivyo vilivyopimwa.
Awali ofa ya
huduma hiyo ilipangwa kumalizika Juni 10 mwaka huu, lakini sasa
imepelekwa mbele hadi Juni 30, ikiwa ni ongezeko la siku 20 zaidi kama
njia ya kuhakikisha kwamba wale wenye nia hiyo wanafanikisha ndoto zao
za kumiliki viwanja.
Akizungumza leo mchana jijini Dar es Salaam,
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema
kwamba wamekuwa wakipokea maombi mengi kutoka kwa Watanzania wenye
uhitaji wa viwanja hivyo, jambo lililowafanya wakae na kuona namna gani
wataongeza siku chache kwa wananchi na wateja wao. Alisema kama
ilivyokuwa mwanzo, wateja wao watalazimika kuchukua fomu za maombi ya
mikopo ya viwanja hivyo katika ofisi yoyote ya Bayport, bila kusahau
wakala wao ambayo ni tawi lolote la Bank of Africa (BOA), huku akitakiwa
kulipa malipo ya awali kuanzia Sh 150,000.
“Kama ilivyokuwa
mwanzo, mara baada ya mteja wetu kuchukua fomu na kulipa Sh 150,000 kwa
kupitia benki ya BOA, ataleta nyaraka zake kwetu na atapatiwa kiwanja
chake, huku gharama za kiwanja cha chini kabisa ni Sh 1,400,000, ambapo
Bayport itamlipia gharama zilizosalia, huku akilazimika kulipia Sh
105,181 kwa mwezi kwa kipindi cha miezi 24,” alisema Mndeme.
Naye
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula
Cheyo, alisema kwamba huduma yao ni muhimu kwa watumishi wa umma,
wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali ambao wote kwa pamoja
wanachotakiwa kufanya ni kuchukua fomu na kuchagua viwanja watakavyo,
kutoka kwenye mradi huo wenye viwanja 1878, huku pia mteja akiweza
kupata kiwanja kwa fedha taslimu ya kuanzia Sh 1,400,000 na kuendelea.
“Viwanja
hivyo vina uwezo wa kujengwa nyumba za kupanga na kupangisha, hoteli na
maduka, vituo vya elimu na ibada, hospitali na kumbi mbalimbali, huku
mradi wa umeme na maji vikiwa vinapatikana ndani ya mradi huo ambao ni
kilomita 50 kutoka Kisutu jijini Dar es Salaam na kilomita 6.5 kutoka
barabara Kuu ya Morogoro,” alisema Cheyo.
Kwa wateja wa malipo ya
fedha taslimu, mara baada ya mtu kulipa malipo ya awali katika akaunti
ya Bayport iliyopo Bank of Africa (BOA) na kukabidhi nakala ya malipo na
fomu za maombi kwa wakala au ofisi ya Bayport, mteja atatengewa eneo
kutokana na maombi yake na kuombwa kumalizia kiasi kilichosalia, huku
hati ya umiliki wa kiwanja akiipata ndani ya siku 90 baada ya kumaliza
malipo yake, na wanaotaka kupata viwanja kwa njia ya mkopo kwa watumishi
wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali, wakipata hati
zao baada ya kumaliza mkopo wao.
No comments:
Post a Comment