Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Ben Pol amesimulia jinsi alivyobishana na marafiki zake kabla ya kuanza safari ya boti ambayo wakati wa kurudi ilizama na kunusurika kifo baharini.
Akizungumza leo, Ben Pol amesema kabla ya safari yao, marafiki zake walimtaka awapigie simu watu wengi zaidi hali ambayo iliibua mabishano yaliyokuja kuwa neema kwao.
“Kabla ya safari marafiki zangu walikuwa wanataka niwaite watu wengi zaidi, yaani tuwaite marafiki wengi. Walikuwa wakiniambia ‘wapigie simu waje hata kumi’, mimi nikawa nawaambia ‘wanangu mimi sitaki kuwaita kwa sababu tutatumia gharama nyingi,” amesema Ben.
“Mimi nilikuwa naangalia kwenye gharama, tukabishana sana wanataka watu waongezeke. Sasa ningekubali kuwaita wangekufa sijui ingekuwaje,” aliongeza muimbaji huyo.
Katika ajali hiyo boti waliyokuwa wamepanda wakitoa kisiwani Mbudya wiki chache zilizopita, ilizama kabisa na wao kusaidia na makoti ya kuogelea ambapo baadaye waliokolewa.
Ben Pol amesema tukio hilo limemfundisha na kumpa moyo wa kuendelea kuwasaidia watu wasiojiweza ikiwa ni njia ya kumshuruku Mungu kwa kuokoa maisha yake.
CHANZO: BONGO 5
No comments:
Post a Comment