HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » GRL YAGAWA MCHE YA MITI MILIONI TANO KWA WANANCHI WA MABAONI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mufindi (DED), Saada Malunde (mwenye hijabu) akipata maelezo kutoka kwa mtaalum wa uzalishaji miche, Prosper Wilbright (pili kulia) ya jinsi Kampuni ya Green Resources Ltd inavyozalisha miche ya miti kitaalamu alipotembelea bustani hiyo ya kuzalisha miche mbalimbali iliyopo katika Kijiji cha Mabaoni wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mabaoni, Sailas Ndenga (kushoto) akipekea funguo ya jengo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Green Resources Ltd, Anthony Kisondella wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Kijiji cha Mabaoni, wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

Green Resources Ltd (GRL) imegawa zaidi ya miche milioni tano kwa wananchi pamoja na kupawatia mafunzo ya namna ya utunzaji na upandaji wa misitu.

Kaimu Mkurugenzi wa GRL, Anthony Kisondella kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Roselyne Mariki, alisema kuwa hekta zinazokadiriwa kufikia 20,000 zimepandwa miti katika mashamba binafsi ya wanavijiji.

Alitoa rai wakati wa kukabidhi jengo la ukumbi na ofisi kwa Kijiji cha Mabaoni, Kata ya Makungu katika Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa jana.

Green Resources Ltd (GRL) ni kampuni tanzu ya Green Resources AS ya Norway, na imewekeza katika sekta ya misitu ikiwa na mashamba makubwa ambapo hekta 17,000 tayari zimepandwa miti katika wilaya za Mufindi na Kilombero.

“Kampuni ya GRL itaendelea kushirikiana kwa dhati na halmashauri za wilaya ya Mufindi na Kilombero na jamii za vijiji ilipowekeza katika kutekeleza miradi inayolenga kuboresha maisha wa wananchi,” alisema.

Kaimu mkurugenzi huyo aliwataka wananchi kutoa ushirikiano unaostahili na michango iliyo ndani ya uwezo wao kama nguvukazi na vifaa kama mawe, matofali na mchanga.

Alisema kuwa mradi wa ujenzi wa jengo la ukumbi na ofisi kwa ajili ya serikali ya Kijiji cha Mabaoni ulianza rasmi Oktoba mwaka jana, ambapo ujenzi wake uligharimu jumla ya shilingi 66,439,456/-.

Aidha, alisema jamii ilishiriki kwa kiasi kikubwa kutoa nguvukazi wakati wa utekelezaji wa mradi huu.

“Jengo hili lina ukumbi wenye uwezo wa kuchukua watu 200 kwa ajili ya kufanyia mikutano, sherehe na semina na vilevile jengo hilo lina vyumba vinne vya ofisi na vyumba viwili vya kuifadhia wahalifu, ” alisema.

Alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo ulisimamiwa kwa niaba ya GRL na shirika linaloitwa ‘Southern Highlands Participatory Organization (SHIPO)’ lenye makao yake makuu mkoani Njombe.

Kampuni ya GRL imekabidhi rasmi Serikali ya Kijiji cha Mabaoni jengo la ukumbi na ofisi mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, ili kama wamiliki waweze kulitumia kulingana na malengo yaliokusudiwa.

“Moja ya mikakati ambayo Kampuni ya GRL imejiwekea ni kushirikiana na jamii kwenye maeneo iliyowekeza kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii katika sekta ya afya, elimu na kadhalika inaotokana na mahitaji na vipaumbele vya jamii husika,” alisema kaimu mkurugenzi mtendaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mufindi (DED), Saada Malunde ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya jengo la ukumbi na ofisi kwa Kijiji cha Mabaoni, aliishukuru kampuni ya GRL kwa msaada huo.

Aidha, DED huyo aliwaasa wananchi wa Kijiji cha Mabaoni kwa kuhakikisha wanatunza vizuri jengo na endapo kutatokea uharibifu wowote, basi watafanya matengenezo yanayotakiwa.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini.

“Na faida ya uwekezaji ni kama haya matunda tunayoyaona leo kwa kijiji cha Mabaoni,” aliongezea.

Naye, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mabaoni, Sailas Ndenga aliishukuru Kampuni ya GRL kwa msaada huo kwa niaba ya wananchi wake na kuahidi kushirikiana na kampuni hiyo kwa lengo la koboresha maisha ya wananchi.

Alisema kuwa wakati anatoa ardhi hiyo kwa kampuni ya GRL, wapo wananchi waliothubutu kumnyoshea vidole kwamba ameuza ardhi ya kijiji kwa mwekezaji, lakini leo wanaona matunda yake.

Aidha, kampuni hiyo ya Green Resources Ltd ina bustani kubwa ya kuzalisha miche iliyopo Kijiji cha Mabaoni.

Mashamba mengine ya miti yapo kwenye vijiji vya Mapanda, Chogo, Ukami, Incomet na Idete kwa Wilaya ya Mufindi na vijiji vya Uchindile, Masagati na Kitete kwa Wilaya ya Kilombero.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: