HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MWANDISHI WA HABARI WA TBC FLORENCY DYAULI AMEFARIKI DUNIA LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



MWANDISHI wa habari mwandamizi wa Shirika la Utangazaji nchini TBC FLORENCY DYAULI (Pichani enzi za uhai wake)amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua.

FRORENCE DYAULI amefariki dunia majira ya saa kumi alfajiri akiwa amelazwa katika hospitali ya RABININSIA MEMORIAL jijini  Dar es Salaam, ambako alikuwa akipata matibabu.

Dyauli alizaliwa  tarehe   27 mwezi wa saba mwaka 1961 na amefariki dunia tarehe   18/06/2015.
Marehemu DYAULI alisoma shule ya msingi   CHANG’OMBE mwaka 1968 hadi 1975.
Alipata elimu ya sekondari mwa 1976 hadi 1979 katika shule ya wasichana KISUTU jijijini Dar es Salaam.
Baadae alijiunga na Chuo cha Uhazili TABORA na kupata cheti katika fani ya katibu muhtasi mwaka 1980 hadi 1981.
Marehemu DYAULI alipata stashahada ya uandishi wa habari  mwaka 1988 katika chuo cha Uandishi wa habari TSJ jijini Dar es Salaam.
Taratibu za mipango ya mazishi tutaendelea kuwajulisha katika taarifa zetu zijazo.

CHANZO: MICHUZI BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: