Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ubora wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala wa baraza hilo Twilumba Mponzi na Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex Nkondola.
Wakurugenzi wa Manejimenti ya NACTE wakiwa kwenye mkutano pamoja na waandishi wa habari uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha EAT, Noah Laltaila akimuuliza swali Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga kwenye mkutano uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Vyuo vilivyofutiwa
usajili ni pamoja na Dar es Salaam College of Clinical Medicine cha jijini Dar
es Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali, Ndatele School of Medical
Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali
na Institute for Information Technology
cha jijini Dar es Salaam pia
chenye namba za usajili REG/EOS/014.
Taassi/vyuo vilivyoshushwa
hadhi baada ya kushindwa kutiza mashart
ni pamoja na Sura Technologies – Dar es Salaam, Institute of
Management and Information Technology – Dar es Salaam, Techno Brain - Dar es
Salaam, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya, Mbozi
School of Nursing – Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO
Anaesthesia School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi.
Vingine ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC
– Songea, CATC – Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga, COTC – Musoma, Dental
Therapists Training Centre – Tanga, Ngudu School of Environmental Health
Sciences – Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.
Kuhusu NACTE
Baraza la Taifa la Elimu
ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129,
kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva
elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu
kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa
kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na
taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
No comments:
Post a Comment