HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » POLISI MKOANI IRINGA WAKAMATA MAGUNIA MATATU YA BANGI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Polisi mkoani Iringa wamefanya msako kali kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na uaslama na kufanyikwa kukamata magunia matatu ya bangi, CD za mafunzo ya jihadi za kialshaababu pamoja na nguzo 35 za umeme mali ya shirika la umeme Tanesco.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Ramadhani Mungi alisema polisi walifanya opresheni kusaka mambo yanayohusu makosa ya jinai na kufanyikwa kukamata maguni ya bangi pamoja na kukamatwa watuhumiwa sugu katika eneo ya njiapanda ya Tosamaganga.

Alisema magunia hayo ya bangi yakiwa yamefungashwa katika mifuko mdogo na misokoto yalikamatwa pamoja na watuhumiwa sugu wawili.

“Watu hawa wamekamatwa wakati wa kiendelea kufunga bangi hizo katika vifungashio mbalimbali pamoja na misokoto,” alielezea kamanda.

Kamanda huyo aliwataja watuhumiwa kuwa ni Steven Sanga na Nicolaus Tweve, ambao alisema ni maarufu sana kwa kuingiza na kusambaza bangi mkoani hapa.


Alisema kuwa Tweve ni maarufu sana kwa kuingiza na kusambaza madawa ya kulevya mkoani hapa na hivi juzi juzi ametoka magereza kwa kosa hilo hilo la kujihusisha na usambaji na uigizaji wa bangi.

“Watu kama hawa wanatuharibia vijana wetu, wanatuharibia pia nguvu kazi,” alisisitiza kamanda.

Kama vile haitoshi, Jeshi la Polisi lilifanyikiwa kukamata nguzo za umeme 35, nyaya za umeme na vifaa vingine vya kufungia umeme katika maeneo mbalimbali vinazodaiwa kuwa mali ya shirika la umeme nchini Tanesco.

Alisema kuwa vifaa hivyo vimekatwa kwa watu binafsi wawili, lakini kutokana na upelelezi kuendelea kamanda huyo hakutaka kuwataji watuhumiwa hao.

Aliongeza kuwa nguzo hizo zilitakiwa kuwepo maeneo ya vijijini ambapo kuna zoezi la kusambaza umeme vijijini, lakini zimekutwa kwa watu binfasi kinyume na sheria.

“Huku ni kurudisha nyuma jitihada za serikali za kusambaza umeme katika mkoa wetu hasa maeneo ya vijijini,” alisema kamanda.

Wakati huouhuo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mbalimbali limewakata watoto wanne wakiwa na CD zinazoonesha mafunzo ya ukatili, kuchinja na kuua ya kialshaababu.

Alisema kuwa watoto hao wanakadriwa kuwa na umri kuanzia 12 hadi 16 na wanaonesha CD hizo katika maeneo mbalimbali.

Alisema CD hizo zimekatwa kutoka kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na polisi inaendelea na uchunguzi kujua watoto hao wamezipata wapi na ni kwa lengo gani na kutakujua baada ya mafunzo hayo watayafania kazi gani.

“CD hizo tumeziangali zinaonesha mafunzo ya kialshaababu yakiwemo kuua, kuchinja pamoja na mambo mengine. CD hizi tumebaini zinaonesha kwa kutumia kompyuta ambayo imefungwa kwa pasiwedi (password). Kama jeshi la polisi hatutaishia hapo tutaendelea na uchunguzi watoto hao CD hizo wanazipata wapi na kwa madhumini gani,” alisema.

Alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu kujihusisha na mambo ya kiuharifu kama vile kusamabza madawa ya kulevya pamoja na uharibifu wa miundo mbinu ya umeme.

Hata hivyo, kamanda huyo ametoa wito kwa umma kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kutoa taarifa pindi wanapoona kuna watu au vitu ambavyo si vya kawaida.

“CD hizi nyingi, bangi ni nyingi lakini vile vile uharibifu wa miuondombinu wa umeme ni mkubwa,” alimalizia kamanda.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: