Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mbunge wa Jimbo la Rombo, Mhe. Joseph Selasini, akiwaonyesha waandishi wa habari mkataba wa ubia kati ya Raia wa China na anayedai ni Mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama.
Na Georgina Misama, MAELEZO-Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameombwa kumwajibisha mara moja Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Bwn. Leonidas Gama kwa kutumia vibaya madaraka yake na kujiingiza kwenye
biashara chafu ya kupora na kuwapa wawekezaji wageni ardhi ya wananchi mkoani humo.
Ombi hilo limetolewa leo na Mbunge wa Rombo, Mkoani Kilimanjaro Mhe. Joseph Selasini
alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari wa Bunge, Mjini Dodoma.
Aidha, Mhe. Selasini ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)
imchunguze mkuu huyo wa mkoa pamoja na watendaji wote wa serikali ambao amedai
wametumia madaraka yao vibaya, kuwatapeli wananchi ardhi na kutumia isivyo halali fedha za
Halmashauri za Wilaya ya Rombo shilingi million 168 kuanzisha kampuni binafsi.
Amesema Mkuu huyo wa Mkoa aliilazimisha halmashauri ya Rombo kutoa fedha hizo shilingi
millioni 168 kuwalipa fidia wanaushirika wa Lokolova waliotoa kwa hiyari yao, kwa Rais
Jakaya Kikwete ardhi heka 140 kwa ajili ya kujenga soko la kisasa.
Amesema hata hivyo, bwana Gama ameshiriki katika kuanzisha kampuni binafsi ya ubia ya
kujenga na kuendesha soko hilo inayomilikiwa na wananchi wawili raia wa China na Mtoto wa
Mkuu huyo wa Mkoa. Kampuni hiyo imeanzishwa bila kushirikisha Halmashauri ya Wilaya ya
Rombo ambayo alitoa fedha za kulipa fidia wala wananchi wa rombo.
Amesema wakati alipokwenda China kuwatafuta wawekezaji hao, Bwn. Gama alitumia fedha za
Halmashauri ya Rombo na nembo ya serikali ya mkoa imetumika katika kuanzisha kampuni hiyo
binafsi.
Mhe. Selasini amesema pia kuwa, Bwn. Gama amefuta ushirika wa Lokolova na kuunyang’anya
ardhi uliokuwa nayo eka 2100 ingawa Waziri Mkuu ameagiza ushirika huo urejeshwa.
Mhe. Selasini aliyeambatana na Mbunge wa Vunjo, Mhe. Augustine Mrema amesema kuwa,
kuna tetesi kwamba kampuni hiyo binafsi imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kulipa fidia
lakini shilingi milioni 168 zilizotolewa na Halmashauri ya Rombo haijulikani zimefanyiwa nini.
Mbunge huyu amesema yeye hapingi uwekezaji katika jimbo la Rombo lakini anataka uwekezaji
huo uwe shirikishi wananchi waukubali na wawe wabia au wanufaike na ajira zinazotokana na
uwekezaji huo.
Ushauri huo ulitolewa pia juzi na Waziri kivuli wa Wizara wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. Halima Mdee wakati akiwasilisha bajeti ya kambi ya upinzani. Pia
Mhe. Mrema amewasilisha leo Hoja binafsi kuhusu suala hilo.
Hata hivyo, Spika, Mheshimiwa Anna Makinda amesema kama alivyoahidi Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Ardhi juzi kuwa hawezi kulitolea jibu suala hilo mpaka ufanywe
uchunguzi kupata ushuhuda na wabunge hao wawe wavumilivu ili wizara iweze kulifuatilia
suala hilo.
No comments:
Post a Comment