Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Moto umeteketeza soko kuu la Masasi(Mkuti) usiku wa kuamkia leo, kwa habari za mwazo zinaeleza kuwa inasemekana kuwa chanzo cha moto huo ni shoti ya Umeme. Wananchi walijaribu kuuzima lakini kutokana na moto huo kuwa mkubwa hadi kupelekea kuwashinda na kilichokuwa kinafanyika baada ya hapo sio kuzima bali ni kuokoa vitu vichache vitakavyopatikanika maeneo yale yote ambapo moto huo bado haujatanda.
Ripota wetu anaeleza kuwa gari la kuzima moto lilichelewa na kufika soko hilo limeishateketea kwa moto. Wakati wa uokoaji huo kuna baadhi ya watu wajeruhiwa na hata watu wengine kuima mali zilizokuwa zikiokolewa hata wengine kubomoa na kuiba. Katika eneo hilo la tukio kumesikika vilio kwa baadhi ya wafanyabiashara wakati soko hilo likiteketea kwa moto.
Endelea kutufuatilia kwa habari zaidi
No comments:
Post a Comment