USAFIRI UNAOTUMIKA KUSAFIRISHA ABIRIA MKOANI GEITA ENEO LA BUSERESERE NI HATARISHI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 
Abiria wakiwa wamekusanywa kwenye buti eneo la kubebea mizigo huku wakiwa sambaba na watoto wadogo.
 Mizigo na Watoto wakiwa wamekusanywa pamoja na mizigo nyuma ya Gari hiyo

Wakazi wa Mkoa wa Geita maeneo ya buseresere na katoro wapo katika hatari kubwa ya maisha yao kutokana na usafiri wanaoutumia kutoka eneo moja kwenda jingine.Mwakilishi wa kikundi cha usalama barabarani Fungo Agustus ametutumia Tukio hili ambalo ni hatari kwa abiria mkoani Geita.Gari ndogo aina ya Pro Box zimeingia kwa wingi mkoani Geita na kutumika kubebea abiria katika mazingira ambayo si salama na ni hatarishi kwa abiria hao.Abiria wamekuwa wakipakiwa kwenye mabuti ya kuwekea mizigo tena kwa msongamano mkubwa.Zifutazo chini ni picha za kinachoendelea kwenye usafirishaji eneo la Buseresere. 

Gari Aina ya Pro Box Ikiwa tayari kusafirisha abiria
 Aina nyingine ya Gari ndogo inayotumika kubebea abiria.

No comments

Powered by Blogger.