WATU 100 WAFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE YA KIJESHI NCHINI INDONESIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Takriban watu 100 wameuawa baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka mapema leo katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.
 Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa tayari miili 49 imepatikana katika eneo la ajali.

 Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
 Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules 130 ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 50 ilipoanguka.
 Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka. Ndege hiyo iliharibu kabisa nyumba ambayo iliangukia katika mji wa Medan, kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
 Picha za runinga na kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Msemaji wa jeshi la angani alisema kuwa rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.

HABARI NA BBC SWAHILI/PICHA NA YAHOO

No comments

Powered by Blogger.