HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » KAMANDA WA POLISI DODOMA AKANUSHA UVUMI WA KUFARIKI DUNIA JOSEPH ELIAZA CHILONGANI ANAYEDAIWA KUPIGWA NA JOBU YUSTOO NDUGAI (MB).

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP akizungumza na vyombo vya habari

Na. Lakia Ndwellah wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Mnamo tarehe 28.7.2015 majira ya jioni JOSEPH ELIAZA CHILONGANI alifika katika kituo cha Polisi Kibaigwa akilalalmika kuwa wakati wakiwa kwenye kampeni za kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge kupitia CCM alishambuliwa kwa fimbo sehemu za kichwani na tumboni na JOBU YUSTOO NDUGAI (MB).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamiz wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema mtu huyo aliyejeruhiwa alipewa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa uchaguzi wa madaktari na matibabu. Amelazwa na anaendelea na matibabu hadi sasa, hali yake anaendelea vizuri. 

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa malalamiko hayo unafanyiwa kazi kwa kupata maelezo ya watu walio kuwa kwenye mkutano huo wa kampeni na ukikamilishwa jalada litapelekwa kwa Wakili wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: