HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » KAMBI MBWANA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE HANDENI VIJIJINI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwandishi wa Habari za Michezo na mdau wa maendeleo ya wilaya ya Handeni, Kambi Mbwana, mwenye fulana ya CCM, akikabidhiwa fomu ya kuwania Ubunge, Jimbo la Handeni Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha Muya, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kulia kwa Mbwana ni Jerome Mhando, mmoja wa wadau waliomsindikiza katika tukio la uchukuaji fomu ya kuwania nafasi ya kuwatumikia wana Handeni. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Kambi Mbwana ajitosa Ubunge Handeni Vijijini
Na Mwandishi Wetu, Handeni
MWANDISHI wa habari za michezo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga, amejitokeza rasmi katika mbio za kuwania ubunge jimbo la Handeni Vijijini kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Makabidhiano hayo ya fomu yalifanyika mbele ya Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha Muya, ikiwa ni siku chache baada ya milango ya uchukuaji fomu za kuwania nafasi za Ubunge na udiwani kufunguliwa rasmi. Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mbwana alisema kwamba ameamua kujitokeza katika mbio hizo za ubunge ili afanyie kwa vitendo yale aliyokuwa anayapenda, hususan katika suala zima la maendeleo, huku wachache wao wakishindwa kuelewa faida ya harakati zake, zikiwapo zile za kuitangaza Handeni kwa njia mbalimbali.
Alisema wilaya yao imekuwa na changamoto kadhaa zinazohitaji nguvu za pamoja katika suala zima la shida ya kubwa ya maji, migogoro ya ardhi, ukosefu wa huduma bora za kijamii, hivyo kunahitajika jitihada na mipango ya pamoja kufanikishaji mambo hayo.
“Nilikuwa kimya kwa siku kadhaa nikiangalia akina nani wapo katika mchakato wa kuhitaji nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Handeni Vijijini na kusikitishwa na watu wasioishi huku na wasiokuwa na uchungu wala dhamira ya kuwakwamua wananchi wakijitokeza kwa wingi kuwania nafasi ya ubunge, inaonyesha wapo kwa maslahi yao zaidi.

“Hii haiwezi kukubalika, ukizingatia kwamba wananchi wameendelea kuishi maisha ya mashaka kwa kukosa maji safi, elimu, afya, michezo, utamaduni na mambo mengine yanayopaswa kufanyiwa kazi kwa kushirikiana na watu wote, wakiwamo viongozi wa kisiasa, watendaji wa serikali na Watanzania kwa ujumla,” alisema Mbwana.

Licha ya kuonekana mpya katika ulingo wa kisiasa hususan kwa nafasi ya ubunge, Mbwana anakumbukwa na kushukuriwa na wengi kutokana na mradi wake wa Tamasha la Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka, kuasisi Taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, bila kusahau kuandika kitabu kinachojulikana kama Dira na Tumaini Jipya Handeni kilichopokewa kwa hisia tofauti, haswa kutokana na kilichoandikwa kwenye kitabu hicho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: