Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwansheria na Kada wa Chama cha Mapinduzi, Emmanuel Makene (katikati) akiwa ameambata na mkewe Dk. Sarah Makene kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya wana CCM Kinondoni kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Kinondoni. Anaepokea fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe. Wengine ni wapambe wa mgombea huyo waliomsindikiza kurejesha fomu hizo leo.
Emmanuel Tamila Makene ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya na Katibu wa Usalama na Maadili taifa wa Umoja wa vijana (UVCCM) akisaini kitabu cha kurejesha fomu huku mkewe Dk Sarah Makene akimwangalia kwa makini na Katibu wa CCM Wilaya akikagua fimu. Dk Sarah Makene ni Daktari katika Hospitali ya Mwananyamala anaeshughulika na wagonjwa wa Ukimwi na Waathirika na dawa za kulevya.
Dk Sarah Makene ni Daktari katika Hospitali ya Mwananyamala anaeshughulika na wagonjwa wa Ukimwi na wWaathirika na dawa za kulevya, akipeana mkono na Katibu wa CCM Wilaya baada ya kupokea fomu za Muwewe.
Makene akiwa na Mkewe Dk Sarah pamoja na rafiki yao baada ya kurudisha fomu.
Makene akiwa na Mkewe Dk Sarah na marafiki zao baada ya kurejesha fomu.
No comments:
Post a Comment