HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MLINZI WA MAHAKAMA AUAWA KIKATILI MKOANI MOROGORO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Watu wasiojulikana wamemuua mtu mmoja anayedaiwa kuwa mlinzi wa Mahakama ya Kinguluwira mjini Morogoro (jina lake halijajulikana bado) kwa kumkata panga kichwani na kunyofoa baadhi ya viungo vyake, kisha kutupa mwili wake katika mashamba ya Pangawe mjini Morogoro.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, mwili huo ulikutwa ukiwa umeharibika vibaya huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa.
Kwa mujibu wa mashuhuda na ndugu wa marehemu wamesema mtu huyo alipotea nyumbani takribani 
siku kumi na mbili zilizopita hadi alipookotwa na wachunga ng`ombe akiwa ameuawa na mwili wake ukiwa umeharibika.
Aidha Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambuka Reli, Adamu Mwamganga amesema kuwa, amepata tarifa hizo kwa wachunga ng`ombe kisha kutoa tarifa kwa Jeshi la Polisi ambapo ameeleza marehemu alikuwa na ugomvi na ndugu zake kuhusu mashamba huenda ndicho chanzo cha kifo chake .
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuuchukua mwili wa marehemu ambao umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti wakati uchunguzi ukiwa bado unaendelea.
CHANZO NA EATV

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: