Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Inabidi kufikiria kwa namna tunavyofikiri kuhusu kazi na juhudi nyingi tunazofanya kuhakikisha kwamba lazima nipate ajira ya kudumu. Inawezekana huko tunakokwenda kusiwe na kitu kinaitwa ajira ya kudumu na kisirudi tena.
Kwa maisha ya sasa kwenye baadhi ya taasisi na taasisi nyingi huko mbele kazi itakuwa na sura mbili unaweza ukaingia kama inalipa uendelee na kama hailipi utokomee mbali. Vivyo hivyo kwa mwajiri atakutizama hivyo kama unampa faida utakaa kama humpi faida atakufungashia virago vyako uelekeee kwenu.
Makampuni mengi yameficha suala hili la ajira ya kudumu hali kwamba wanajua halipo. Watu wanahitaji maisha huru wakati wanafikiria kazi na taaluma zao na wapi wafanye kazi kwa wakati gani. Ninaweza kuendelea na kuendelea jinsi maafisa waajiri walivyo na wanafikiri nini hasa?
Kwa mfano wakati wanatafuta mtu ambaye anatakiwa kusimamia fedha wanaangalia mambo mengi hasa unafanyaje maamuzi, na je ukiona hela nyingi unafanyaje? Na je ulishawahi kusimamia fedha na ulizitunzaje? Kama ni za kwako au kama si za kwako? Haijalishi kama unafikiri kazi hiyo unaiweza klakini ukakosa ujuzi husika kwenye kazi hiyo sidhani kama unaweza ukapewa jukumu hilo.
Watu kwenye umri ambao wanaonekana kukomaa kifikra, uzoefu na hekima mara nyingi huwa hawachukulii kazi kwa umakini mkubwa sana. Kazi si kitu pekee cha maisha yao, kwahiyo kazi ni kazi tu.Hivyo wanapotafuta kazi huwa si kama kwamba wanataka kufanya kazi sana bali kuna kitu kingine wanakitafuta, labda namna gani wataweza kuendesha miradi yao kwahiyo hapo anataka kujua tu mambo yanafanyikaje. Hata utendaji wao huwa wa kawaida sana, hutegemea vijana au watu walio chini yao sana ila wao hupata sifa ya utendaji bora.
Hivyo unapoangalia ajira ya kudumu, utagundua ni kitu ambacho ni kigumu na wala hakiwezekani kwa urahisi huo. Lazima utafute mbadala wa maisha yako, kwani ukisubiri ajira ya kudumu inawezekana usiipate na pindi utakapoipata hiyo unayodhani ni ya kudumu kuna kiwango cha maisha hautakuwa zaidi ya hapo. Pale tu utakapoweza kufanya mbadala wake utashangaa maisha yanaanza kubadilika na kuanza kusogea hatua nyingine.
Mashirika ya kiserikali sana ndio yanayoweza kukuweka kwa muda mrefu kwakuwa wao hawaangalii sana au hawaangalii kabisa faida bali kutumikia jamii. Ndio maana viwango vya rushwa ni vikubwa sana kwakuwa hawawezi kufanikiwa kwa vile unavyowaona mpaka wafanye kitu ambacho ni tofauti sana au kabisa na mshahara wao. Na sio wote wanaokwenda kufanya kazi huko ni kwasababu ya kazi bali ni kwasababu ya kupata vitu au mipango zaidi ya kazi yenyewe.
Kuna mtu mmoja alisema kuwa mshahara hauwezi kukufanya tajiri na wala hakuna mwajiri ambaye anatamani wewe uwe na maisha ya kujitegemea atahakikisha mshahara wako unakidhi maisha ya kila siku ili uweze kufanya kazi kila siku. Akili yako ndio mwokozi wako, ukikaa kusubiri kupandishwa cheo na mshahara utasubiri sana.
Ukianza kujifunza kufanya zaidi ya kazi tu kwa mwajiri wako na kuangalia fursa nyingine, maisha bora hayataweza kupatikana na wala wanasiasa hawawezi kukupatia ila wao wanayaishi kila siku wanakuhitaji wewe uwasaidie kufika huko.
Je ajira yako unaitazamaje? Kama ni ya kudumu umepiga mahesabu ya utafikia wapi wakati wa kustaafu na utakuwa na hali gani? Maaana hauna njia nyingine, si umepata ajira ya kudumu? Inabidi tuongeze upeo wetu wa kufikiri ili kutoka hapa tulipo bila kufanya hivyo. Kuna maisha tutaendelea kuyasikia redioni au kusoma kwenye magazeti. Ukibadilisha kufikiri kwako utabadilisha ajira yako na kufanya mambo yenye tija kwa kizazi cha na maisha yako ya baadaye.



No comments:
Post a Comment