Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Lugha hiyo chafu ambayo
inajidhihirisha kwa matusi ya wazi, maneno ya uchochezi, kashfa, kejeli, dharau
na udhalilishaji wa kada mbalimbali za kijamii wakiwemo viongozi wa kitaifa
inaonesha wazi kulenga katika kuigawa jamii na kufifisha amani, upendo,
uzalendo na ustaarabu tuliokuwa nao watanzania.
Ieleweke kwamba kwa mujibu
wa misingi ya Sanaa Duniani kote kazi zote za Sanaa zinapaswa ziwe ni zenye
kuonya, kuelimisha, kuadabisha, kukosoa, kuburudisha, kuhamasisha na kuchochea
maendeleo chanya katika jamii na siyo kuigawa au kuivuruga jamii.
Ndiyo maana msanii anayefanya kazi zake kwa kuzingatia misingi ya Sanaa anatambuliwa kuwa ni kioo cha jamii, kiongozi na pia ni mwalimu wa yale yote yaliyo mema katika jamii inayomzunguka.
Kinyume na misingi hiyo ya
Sanaa, baadhi ya Wasanii, studio za kurekodia na kutengenezea muziki, vyombo
vya habari vya kielektroniki na mitandao ya kijamii ama kwa kutumiwa au kwa
utashi wao binafsi wamekuwa wakijihusisha na Sanaa zenye viashiria vya
uchochezi na kuvunja misingi ya weledi katika Sanaa hususan katika kipindi hiki
cha kampeni na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.
Aidha, baadhi ya Wasanii
wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya vyama vya Siasa au wagombea na kujikuta
wakitumiwa vibaya na kuvunja misingi ya Sanaa kwa faida za kisiasa. BASATA linapenda
kutoa maagizo yafuatayo:
1.
Wasanii wana haki zote za kikatiba na kidemokrasia
kushiriki shughuli za Siasa lakini wanawajibika
kwa kiwango cha hali ya juu kulinda misingi ya weledi, maadili, miiko na hadhi yao kama
inavyofanyika katika tasnia zingine.
2.
Wasanii wanapaswa kutambua kwamba kuna maisha
na Taifa baada ya uchaguzi mkuu. Umoja wa kitaifa na umoja baina ya wasanii wa
kada zote za Sanaa ndiyo utakuwa msingi mkuu wa kuendelea kusukuma gurudumu la
maendeleo ya Sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla pasipo kugawanyika katika
misingi ya itikadi za kisiasa
3.
Wasanii wasitumie nafasi na umaarufu wao
kuligawa taifa, kukashifu viongozi wa kitaifa, kudharau mamlaka, vyama na
makundi mbalimbali katika jamii kwa kile kinachoitwa ushabiki wa kisiasa. Ieleweke
kuwa Serikali haitafumbia macho wale wote watakovunja sheria, kanuni na taratibu.
Tukumbuke kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.
4.
Ijulikane kuwa wasanii kama kundi muhimu
katika kipindi cha kampeni za kisiasa ni sawa na watu wengine wanaopewa kazi
ili kutimiza lengo lililokusudiwa. Wasanii wasitumiwe kama vyombo tofauti na
watu wengine.
BASATA linatoa onyo kali
kwa msanii yeyote atakayeendelea kukaidi, kuvunja maadili na kusambaza kwa njia
yoyote ile kazi ya Sanaa yenye ukengeufu wa maadili.
BASATA linawatakia wasanii
wote utekelezaji mwema wa maagizo haya lakini kubwa kuliko yote kutambua kwamba
tunatakiwa kujenga mshikamano, umoja wa kitaifa na kustawisha amani tuliyonayo
ambapo ikitoweka itaathiri ufanisi wa Wasanii na kuirejesha itatugharimu sana.
Sanaa itumike kulinda
amani, kujenga upendo, umoja wa kitaifa na mshikamano baina ya makundi
mbalimbali ya kijamii.
SANAA NI KAZI TUIKUZE,
TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey
L. Mngereza
KATIBU
MTENDAJI, BASATA
No comments:
Post a Comment