HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MHUBIRI MAARUFU WA NIGERIA TB JOSHUA ATUA DAR ES SALAAM KUSHUHUDIA DKT MAGUFULI AKIAPISHWA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
Picha na Freddy Maro

Rais mteule wa awamu ya tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli alimpokea Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria  TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa


Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua jijini Dar es salaam leo  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: