Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Katibu Mkuu
Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo
pichani) beji yenye jina lake ambayo amewaagiza watumishi wa Umma kuivaa
wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. Balozi Sefue alifanya mkutano na
waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana na kutoa taarifa ya
Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office(SFO) dhidi ya Standard Bank.
Na Anna Nkinda – Maelezo
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi.
Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine.
Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao.

“Nimeamua kuonyesha mfano kwa vitendo kufuatia agizo
nililolitoa kwa watumishi wa Umma kwa kuvaa beji inayonitambulisha jina langu ,
nilisema nitakuwa wa kwanza kuvaa jina langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma
atakuwa na mashaka ajue mimi nimeshalivaa”.
“Mtumishi wa umma anapomuhudumia mwananchi
ni lazima ajue amehudumiwa na nani, mtumishi wa Umma akifanya kazi zake kwa
kutenda haki sidhani kama ataogopa kuvaa beji inayomtambulisha jina lake hivyo
basi kama nilivyoagiza watumishi wote wa Umma mvae beji zinazowatambulisha
majina yenu”, alisisitiza Mhe. Balozi Sefue.
Mhe. Balozi Sefue alifanya mkutano na
waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya Serikali
kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.

No comments:
Post a Comment