Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Fisi hao wawili walimshambulia kwa kumng’ata Gamalaya maeneo mbalimbali ya mwili na kusababisha kifo chake, huku wakimjeruhi Ngeleja mikono na miguu.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Magharibi, Charles Msilanga alisema jana (juzi) kuwa baada ya polisi kumpiga risasi fisi mmoja na kumuua, mwingine alikimbia.
Alisema wanaendelea kumsaka fisi huyo ili kuzuia madhara zaidi kwa wakazi wa kitongoji hicho.
“Fisi aliyekimbia anaweza kuleta madhara kwa watu na ndiyo maana tunamsaka kwa udi na uvumba,” alisema Msilanga.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Iddi Cheyo alisema Gamalaya alifariki dunia baada ya kukaa muda mrefu bila matibabu tangu aliposhambuliwa na fisi hao.
Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho, Sophia William na Juma Kapambala walisema tukio hilo limewastaajabisha kwani kwa miaka mingi wanafanya shughuli zao ndani ya msitu huo bila kushambuliwa na wanyama.
No comments:
Post a Comment