Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Na
Mwadishi Wetu
CHAMA cha Wananchi CUF
kinatarajiwa kukutana katika kikao cha Baraza Kuu Taifa la Uongozi jumamosi
ijayo, ajenda Kuu ikiwa ni hali ya kisiasa Zanzibar baada ya uchaguzi wa
marudio uliyofanyika Machi 20, mwaka huu.
Kikao hicho ambacho kinakuja
huku baadhi ya wanachama wa chama hicho wakionekana kama wamechanganyikiwa
kutoka na kususia Uchaguzi huku na kupelekea CCM kujinyakulia ushindi katika
nafasi zote kinategewa kutoka na azimio zito juu ya hali ya kisaisa visiwani
hapa.
“Ndio tunategemeo kukaa siku
ya Jumamosi mwishoni wiki hii na suala la hali ya kisaisa litachukua mda kubwa
kuzungumzwa” kilisema chanzo chetu cha kuaminika.
Chanzo hicho kilisema pia
wajumbe watajadili mambo mengine, wakati huu ambapo wananchi wanahamu ya kujua
kinachoendelea katika chama kwa hiyo kupitia baraza hilo wanategemea kuwapa
mwanga wapi wanaelekea.
Kilifahamisha kwamba
kutokana na hali ilivyo sasa hasa tangu kutangazwa Dk. Ali Muhammed Shein
kuongoza tena Zanzibar wanachama wanachama wao hawajui nini hatma ya chama chao
pamoja wao wenyewe.
“Lazima tutoke na kitu
ambacho kitaweza kuwanyanyua kivyengine kabisaa wafuasi wetu kwani hatuwezi
kustahamilia na dhulma hii hivi hivi” kilitueleza chanzo chetu.
Hali ya wasi wasi na ghofu
kubwa imetanda miongoni mwa wanacuf kutokana kuongezeka kukamatwa kwa viongozi
pamoja na wanachama wa CUF katika maeneo mbali mbali Visiwani hapa.
Kiujumla hali ya kisiasa
viswani hapa imekuwa ya kuti hofu baadhi ya viongozi na wanachama maarufu wa
CUF na kupelekea wengine kuaza kukimbia majumba yao.
Tokea kabla na baada ya uchaguzi
wa marejeo takwimu zinaonesha wanachama zaidi ya 80 wamekamatwa kwa
tuhuma mbali mbali ikiwemo, Uchomaji moto majengo ya serikali na makaazi ya
watu pamoja na uripuaji na utegaji mabomu katika maeneo tafauti Unguja na
Pemba.
Kutokana na kamata kamata hiyo
baadhi wana CUF wanataka kujua hatma yao nini na nini chama chao kinawaeleza.
Katika mitaa mingi hasaa
maeneo ambayo chama hicho kilijinyakulia majimbo katika uchaguzi ambao ulifutwa
hapo October 25 mwaka jana wamekuwa wakijiuliza wapi wanaelekea.
Kikao cha mwisho cha baraza
Kuu kilicho fanyika kilikaliwa Novemba mwaka jana ambacho kiliamua kususia kwa
uchaguzi wa marejeo ambayo ulifanyika Mach 20 mwaka huu.



No comments:
Post a Comment