JESHI LA ULINZI LA
WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA
UHUSIANO.
Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi
ulioenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani
Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi
marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20 Machi, 2016
Habari hizo siyo za
kweli na zina lengo la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani
Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu. Hivyo
hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu
awali. Taarifa hizo zipuuzwe,zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.
JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena
kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama
wa nchi yetu, kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.
Imetolewa na
Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P
9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.
No comments:
Post a Comment