Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Dodoma
ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani kama kituo chenye reli ya
kati na karakana ya reli. Tangu 1912 imekuwa makao makuu ya mkoa. 1913 Dodoma
ilikuwa na posta, simu, hoteli na maduka 26 (moja la mzungu, mengine ya Wahindi
na Waarabu). Kikosi cha polisi kilikuwa na askari 59
Dodoma ni mji wa
Tanzania ya kati. Imetangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka
1973. Hali halisi makao ya kikazi ya serikali ya Tanzania yako Dar Es Salaam pia
ikulu halisi ya rais. Lakini bunge
hukutana Dodoma na sehemu za ofisi za wizara kadhaa zimepelekwa Dodoma. Mji ni pia
makao makuu ya Mkoa
wa Dodoma na Wilaya ya Dodoma.
Eneo la mji liko 1135 m juu ya UB. Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa
2,083,588 mwaka 2012. Kiuchumi ni kitovu cha biashara ya kilimo cha karanga,
maharagwe na alizeti, pamoja na mifugo na kuku.
Asili
ya jina
Neno
"Dodoma" linasemekana kumetokana na neno la kigogo
"dodomia" kufuatili historia kwamba zamani kuna tembo alikuja pale
mjini akakita nyayo zake ardhini akiacha alama ya nyayo zake zimedidimia
Mkoa wa Dodoma uko katikati ya Tanzania umepakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida. Sehemu
kubwa ya eneo lake ni nyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB.
Eneo lote la mkoa lina
41,310 km². Kuna wilaya saba
zifuatazo:
Wilaya ya Bahi, Wilaya ya Chamwino, Wilaya ya Chemba, Wilaya ya Dodoma Mjini, Wilaya ya Kondoa, Wilaya ya Kongwa, Wilaya ya Mpwapwa.
Wilaya ya awali ya Dodoma Vijijini imegawiwa kwa wilaya mpya za Chamwino na Bahi.
Katika sensa ya mwaka
2012, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ilihesabiwa kuwa 2,083,588.
Mnamo Machi 2012 ilianzishwa wilaya mpya ya Chemba
Dodoma
imeendelea kuwa mji mdogo mpaka kutangazwa kuwa mji mkuu. Azimio hili lilileta
ujenzi na maofisi kadhaa ya serikali. Kwa ujumla uhamisho unaendelea kuchelewa
kwa sababu mbalimbali; sababu muhimu ni ya kwamba watumishi wa serikali na
wanasiasa walio wengi hawapendi kuondoka katika jiji halisi na kuhamia mji
mdogo ambao ni mbali sana na mazingira waliyoyazoea. Menginevyo kuna matatizo
ya kifedha ambayo yamesaidia haidi sasa kutangaza nia ya kuhami lakini kubaki
palepale
Mawasiliano
Mawasiliano ni mazuri kwa
barabara ya lami kuanzia mji
wa Dodoma kwenda Morogoro
- Daressalaam,
barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya
Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya
"Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini (Arusha - Kondoa)
kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya Reli ya Kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma yenye
matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege.
Wakazi na
utamaduni
Idadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo. Kondoa kuna warangi, waburunge, Wangulu na pia Wasandawe
wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Wanasemekana ya kwamba babu zao
wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia
sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi
inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini. Kongwa kuna
Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na Mpwapwa
kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru.
No comments:
Post a Comment