Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar
es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi
nyingine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassimu
Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi wakwanza kushoto na
Wamwisho kulia ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi aliyekuwa Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na viongozi Wakuu wa Ulinzi na Usalama nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Makatibu Wakuu wa
Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Manaibu Katibu
Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU.
PICHA NA IKULU.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA
RAIS IKULU
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Mhandisi John
William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Hafla ya kuapishwa
Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Wakuu
wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu.
Balozi Kijazi
ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Balozi wa Tanzania
nchini India, anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi
nyingine.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ameagana na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) anayemaliza muda
wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo
mengine amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote
alichokuwepo hapa nchini.
Kwa upande wake Bi.
Joyce Mends-Cole amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na
Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani migogoro ya kisiasa ambayo
husababisha watu wake kuwa wakimbizi.
Pia amepongeza
kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa,
kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao umesababisha idadi kubwa ya
wakimbizi kukimbilia Tanzania.
Hata hivyo amesema
idadi ya wakimbizi wanaokimbilia Tanzania imepungua kutoka wakimbizi 3,000
waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati Mgogoro wa Burundi ulipoanza
hadi kufikia wakimbizi takribani 1,000 wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi
sasa.
Aidha, Bi. Joyce
Mends-Cole amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi cha
miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahidi kuwa Balozi wa kuitangaza
vyema Tanzania.
Gerson
Msigwa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
07 Machi,
2016
No comments:
Post a Comment