Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC.
Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani Arusha.
Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani Arusha,(katikati) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini,akiwa na Mawaaziri wa Nchi za Jumuiya hiyo,{Picha na Ikulu.]
No comments:
Post a Comment