Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
GARI aina ya Hiace limetumbukia baharini
eneo la Ferry jijini Dar es Salaam mapema leo saakumi na moja alfajiri Aprili
20, 2016 na habari za mwanzo zinasema watu wawili mwanamke na mwanamme
wanahofiwa kufa maji.
Mwili wa Mmoja wa watu hao ukitolewa mara baada
ya kupatikana majini, juhudi za kuutafuta mwili mwingine zinaendelea.
Mashuhuda wanasema, wapiga mbizi kutoka Jeshi
la Ulinzi la Wananchi JWTZ, kikosi cha navy, wamefanikiwa kuokoa mwili wa
mwanamume na kazi ya kutafuta maiti ya mwanamke inaendelea.
Mashuhuda wanasema,
Hiace hiyo ilitumbukia baharini kutoka kwenye kivuko (Ferry) baada ya
gari ilo kuvuka kwenye msitari wa magari yapotakiwa kuishia na ndipo gari
likatumbukia na gari hilo bado hazijapatikana.Kwenye majira ya saa tatu
waliweza kufanikisha kupata mwili wa mwanaume aliyekuwa kwenye hilo gari aian
ya Hiace.
Boti ya mwendo kasi ya JWTZ, ikiwa na
wazamiaji imeonekana eneo la pwani ya magogoni ikiwa kwenye kazi ya kutafuta
gari pamoja na huyo mama aliyebakia kwenye gari hilo.
No comments:
Post a Comment