HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » TAKUKURU WATOA TAMKO KUHUSU MAHAKAMA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na matamshi yaliyotolewa na Leonard Swai, Wakili wa TAKUKURU aliyenukuliwa kwenye vyombo vya Habari tarehe 15/4/2016 kuhusiana na hali ya Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wakili huyo alinukuliwa akisema kuwa “Kuna Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu” baada ya kutolewa hukumu ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Bw. William Mhando ambaye alionekana hana hatia.
Wakili Leonard Swai si msemaji Rasmi wa Taasisi hivyo matamshi aliyoyatoa si msimamo wa TAKUKURU kuhusu Mahakama. Tunaiomba Idara ya Mahakama na jamii kwa ujumla itambue kuwa matamshi hayo aliyoyatoa ni maoni yake binafsi.
TAKUKURU ina jukumu la kisheria la Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mahakama ni muhimili wa Serikali unaotoa haki. Tunaamini kila Taasisi itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo ya Sheria zilizopo.
TAKUKURU inaheshimu uhuru na mamlaka ya Mahakama na itaendelea kufanya hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake.

IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO, 
TAKUKURU MAKAO MAKUU
20 April, 2016

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: