HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » WATUMISHI WA MANISPAA YA DODOMA WAMPOTEZA NAIBU WAZIRI WA OFISI YA RAIS (TAMISEMI)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Msafara wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo jana asubuhi ulipotea njia kutokana na watumishi wa Manispaa ya Dodoma kutojua eneo ambalo waziri huyo alikuwa analitembelea.
 
Waziri Jafo alikuwa amepanga kufanya ziara kwenye Shule ya Msingi ya Nzuguni B kwa lengo la kuangalia mapungufu, hasa tatizo la uhaba wa madawati, lakini hakufika kama alivyotarajia kutokana na watumishi hao kutojua eneo ambalo shule hiyo iko.
 
Shule hiyo haijawahi kutembelewa na ofisa elimu tangu mwaka 2007 licha ya kuwa kilomita 6 kutoka katikati ya mji.

Naibu Waziri alikasirishwa na kitendo hicho akawataka watumishi wa idara ya Elimu wajipime kama wanastahili kuendelea kufanya kazi.

“Mstahiki Meya, mimi niliona wazi kuwa watumishi wako wananipoteza," alisema Waziri Jafo.
 
"Nimechukia sana na hawa watu. Tatizo lao ni kwamba hawajawahi kuja katika shule hii tangu mwaka 2007, lakini wamekaa ofisini tu. Ikiwezekana waondolewe na kupelekwa vijijini,” alisema Jafo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: