Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Unadhani kuwa unajua kila kitu kuhusu mume wa maisha yako? Mahusiano mengi hukoma kwa sababu ya masuala ya mawasiliano, uongo au shakhsia zisizoendana. Mengine hufikia kikomo kwa sababu wanandoa hawakuchukua muda kujuana.
Famasia yako ya Ndoa Maridhawa imekuletea mambo 10 ambayo unatakiwa
kuyajua kuhusu mwanaume wa maisha yako kabla hujachukua hatua zaidi. Iwapo
unayajua baadhi, basi endelea kufuatilia zaidi na zaidi:
1. MALENGO YA KWELI YA KAZI YAKE
Huwenda unaijua kazi yake… lakini unajua kuhusu kazi ya ndoto yake?
Unajuaje iwapo atabadili kazi yake baada ya miaka 5? Tambua mapema iwapo mumeo
anataka kuwa meneja, kibarua au mkurugenzi wa kampuni au shirika. Anaweza akawa
na wazo la kumiliki biashara zake mwenyewe.
2. RADIAMALI YAKE (reaction):
Mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia: “Unaweza kujua kuhusu mtu
fulani kwa kutazama namna anavyoshughulikia mambo”. Kauli hii inatufundisha
kujua kuhusu ghadhabu, hasira na subira ya mtu husika. Hili linaweza kukuonesha
namna mtu huyo alivyo. Kupitia radiamali ya mtu ndipo unapoweza kujua
silka yake. Lizingatie hilo.
3. ENEO ANALOPENDA ZAIDI DUNIANI
Tambua eneo analolipenda zaidi katika maisha yake, na ambalo
humpatia furaha zaidi. Wakati fulani utaweza kutumia fursa hiyo kumfanya kuwa
mwenye furaha.
Kwa mfano, mimi ninapenda sana mkoa wa Kigoma… Sio tu kwa sababu ni
kwetu, lakini kwa sababu kuna mambo mengi yenye kuijaza kumbukumbu ya maisha
yangu kiasi kwamba huhisi ombwe nisipoyaona mambo hayo.




No comments:
Post a Comment