Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani Tanga mara baada ya kutembelea eneo la Zed B ambapo wamehamia wananchi wa Mtaa wa Kibatini kulipotokea mauaji wa watu wanane kwa kuchinjwa ambapo aliongozana na wabunge wa mkoa wa Tanga kuwapa pole wahanga wa tukio hilo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitazama vitu vya wahanga wa tukio la mauaji lililotokea kijiji cha kibatini juzi akiwa na wabunge wa mkoa wa Tanga kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nchi za Nje na Ndani
Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nchi za Nje na Ndani akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la Zed B ambalo wamehamia baadhi ya wananchi walionusurika tukio la mauaji ya watu wanane waliochinjwa juzi kwenye Mtaa wa Kibatini wilaya ya Tanga
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatembelea wananchi hao kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge mambo ya Ndani na Nje ,Balozi Adadi Rajabu na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM)
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mustapha Selebosi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya wabunge wa mkoa wa Tanga kutembelea wananchi waliohamia eneo la Zed B baada ya kuhama makazi yao ya Mtaa wa Kibatini kutokana na kutoka mauaji ya watu wanane waliochinjwa juzi na watu wasiojulikana
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) wakimpa pole mmoja wa wajane ambaye mumewe alichinjwa kwenye tukio la mauaji ya kinyama ya kuchinjwa kwa wakazi wanane wa mtaa wa kibatini na watu wasiojulikana ambao walihamia usikui wa manane
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimuakiwapa pole mmoja wa wafiwa katika tukio hilo la mauaji
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa na mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso wakimsikiliza mmmoja wa wajane waliwapoteza wanaume zao kwenye mauaji ya kinyama ya kuchinjwa watu wanane yaliyotokea mtaa wa kibatini jijini Tanga
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru akimfariji mmoja wakina mama ambaye mumewe aliuwawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment