Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sheriff Hamad akiwapungia mkono baaadhi ya wananchama waliofika uwanja wa ndege zanzibar kumpokea akitokea Marekani.
Maalim Seif
Shari Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF akisalimiana na
baadhi ya viongozi waliofika uwanja wa ndege wa Kimataifa Abeid Aman
Karume kumpokea. (Picha na Talib Ussi).
Na Talib Ussi, Zanzibar
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif
Hamad amerejea Nchini leo akitokea katika ziara zake za
Ughaibuni amewataka wanachi na wanachama wa chama
hicho kuendelea kuwa na subra.
Maalim ameyaeleza hayo nyumbani kwake wakati akitoa salamu kwa
wananchgama waliokua kusanya hapo na kuomba kuelezwa chochote.
“Tumekutana na watu muhimu katika safari yetu na imekuwa na
mafanikio makubwa lakini ni mapema kuwaeleza nini kinaendelea” alieleza Maalim
Seif.
Alisema kuwa katika safari yake hiyo amepokewa vizuri na kueleza
matatizo ya kubakwa kwa demokrasia Zanzibar na wote aliokutana nao
alidai wamemfahamu.
“Ni vyema tukaendelea kuwa subra huku mambo yetu yakifuatiliwa kwa
karibu mnoo” alieleza Maalim Seif.
Malim Seif alifika Kiwanja cha ndege Zanzibar munamo saa 11;30n za
jioni akiongozana na wajumbe ujumbe wake na walinzi wake waliandamana katika
ziara yake hiyo.
Mapema baadhi ya viongozi wa chama hicho walifika kiwan jani hapo
kwa ajili ya kumpokea wakiongozwa na aliyekuwa Mgombea mwenza wa Ukawa Juma
Duni Haji.
Akimkaribisha Maalim Seif Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF Salim
Biman alimueleza maalimu kwamba wanancha leo walijipanga kuja kumpokea mapokezi
makubwa lakini alidai waliwazuia.
“Tumewaambia muda ukifika watakuja kumpokea kwa kishindo lakini
kwanza watulie” alieleza Biman
Katika ziarav hiyo Maalim Seif alienda Uengereza, Ubeligiji,
Uholanzi na baadae kuhudhuria mkutano Mkuu wa chama cha Democratic wa kumteua
mgombea wao Hilary Clinton huko Marekani.



No comments:
Post a Comment