HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » Cristiano Ronaldo: Kutoka kuishi hostel mpaka kumiliki Pestana CR7 Hotels

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mnamo mwaka 2001, kijana wa miaka 16 Cristiano Ronaldo alikuwa akipanda treni kutoka hostel mpaka mazoezini kila siku, wakati huo akiwa mchezaji wa Sporting CP Academy  – akiwa na matumaini ya kupata angalau Euro 1000 kwa mwezi – akiwa anaishi kwenye hostel na wachezaji wenzie.

Residencial Dom Jose, ndio jina la hostel ambayo ilikuwa karibu na mnara maarufu wa jiji la Lisbon Marques de Pombal, hostel hiyo mpaka leo hii ipo. Ilikuwa ni safari ya kila siku ya takribani dakika 15 kwa kijana huyu wa kireno.

 Leo hii miaka takribani 15 baadae, Cristiano Ronaldo anarejea Ureno akiwa mchezaji tajiri zaidi duniani – akiwa na kikosi cha Real Madrid ambacho kinaumana na Sporting CP katika mchezo wa Champions League – wamefikia katika hotel ya The Pestana CR7, hotel ya hadhi ya juu inayomilikiwa na Ronaldo, iliyopo pembezoni mwa pwani ya jiji hilo. Hili pekee linakuonyesha umbali aliotoka kijana huyu miaka 15 iliyopita mpaka sasa.
Pestana CR7 – hotel ambayo wamefikia Real Madrid ni zaidi ya biashara kwa Ronaldo, hii ni pension yake baada ya kazi kubwa anayoifanya. Tayari mpaka sasa ameshafungua nyingine katika kisiwa cha Madeira, eneo alilozaliwa.

Wale waliomuangalia tangu akiwa anahangaika kutafuta nafasi mpaka kufikia mafanikio makubwa akiwa mmoja wa watu mashuhuri zaidi na makombe matatu ya ulaya,  3 Ballon d’Ors, kombe la Euro, miongoni mwa mafanikio yake, leo usiku watapata nafasi nyingine ya kumshuhudia shujaa wao katika uwanja wa Estadio Jose Alvalade akiiongoza Real Madrid vs Sporting CP katika jaribio lingine la kuelekea kwenye utawala mwingine wa soka la ulaya.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: