Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Dr Mwele Malecela, ametoa kauli yake baada ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Dkt John Magufuli, Ijumaa hii.
Kutenguliwa kwake kumekuja siku moja tu baada ya kuzungumza na waandishi na kudai kuwepo kwa virusi vya Zika nchini. Alisema kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti walioufanya, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi hivyo. Taarifa yake, ilikuja kukanushwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Akijibu tweet iliyosema, ” Pole sana @mwelentuli safari yako na isonge mbele Dada,” Dr Mwele amesema, “Ahsante na itasonga kwa msaada wa Mungu.”
Tweet nyingine alijibu: Ahsante Mathew. Nilipewa dhamana nimetumikia ninamshukuru Mungu kwa nafasi ya kutumikia WaTanzania kupitia utafiti.”




No comments:
Post a Comment