HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » JE WATAKA KUJUA: WACHINA WANATUMIA ZAIDI YA CHOPSTICKS (VIJITI VYA KULIA CHAKULA) VIPATAVYO BILLION 80 KWA MWAKA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kwa mwaka mmoja Wachina wanatumia zaidi ya chopsticks (vijiti vya kulia chakula) vipatavyo Billion 80. (80,000,000,000+). Kiasi hicho cha chopstick kimesababisha kukatwa kwa zaidi ya miti mikubwa ipatayo million 20 kwa mwaka. Katika kiasi hicho Chopsticks Billion 57 zinazalishwa nchini China na zaidi ya Billion 23 zinaagizwa kutoka Marekani.

Kuhusu vijiti vya kulia vya kichina na vijiko, baadhi ya watu wanaona kuwa, China ni nchi ya kilimo, vyakula vikuu vya China ni nafaka na mboga, hivyo watu wanatumia vijiti kula chakula. Na nchi za magharibi nyingi zilikuwa ni nchi za kufuga mifugo, vyakula vikuu vyao ni vya nyama, hivyo wanapendelea kutumia vijiko. Mbali na hayo, wachina wa familia moja hula vyakula pamoja, ambapo vitoweo huwekwa kwenye sahani moja moja kwenye meza moja, hivyo watu wanatumia vijiti vya kulia kuchukua kitoweo kila mara. Na kwa wazungu, kila mtu ale vyakula vyake kwenye sahani yake. Jambo linalosisitizwa ni kuwa, ni mwiko kwa wachina kupachika vijiti vya kulia kwenye wali au kupiga bakuli kwa vijiti vya kulia.

Imeandaliwa na Moses Mutente

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: