HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » MKUU WA CHUO MSTAAFU APANDISHWA KIZIMBANI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo(LGTI), Emanuel Gibali na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kwa kosa la kupokea rushwa ya Sh 12.4 milioni kutoka Manispaa ya Morogoro.
Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Godfrey Pius, Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru), Biswaro Biswaro alisema washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa manne ambayo waliyafanya Septemba, 2015 chuoni hapo.
Biswaro aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Utafiti ,Ushauri na Mafunzo Mafupi, Benjamen Magori na Mhasibu wa Chuo hicho, Eliakundi Samanya.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Pius alisema dhamana zipo wazi na kutoa masharti kuwa kila mmoja anatakiwa kujidhamini mwenyewe kwa mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi ya Sh 2 milioni na dhamini moja mwenye barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa.
Watuhumiwa wote watatu wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza msharti ya dhamana na kesi yao itatajwa tena januari 18, waka 2017 .

Chanzo: Mwananchi

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: