HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » SUMU YA PENZI SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO (25)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Nilikumbuka kuwa ndani yake kuna zile meseji za kukutana gesti na uchafu wa aina hiyo, ambao wote uliashiria kuwa nilikuwa naisaliti ndoa yangu.
Nilijikuta tu nikipiga magoti na kumuomba msamaha mume wangu kabla hata hajamaliza kusoma zile meseji. Lakini kwa hasira alizokuwa nazo akanipiga kibao hadi nikaanguka chini. 
Hakuwahi kunipiga hata siku moja tangu nianze kuishi naye, siku zote alikuwa akinichukulia kama malkia wake, lakini mpaka siku hiyo aliamua kunipiga basi nilijua lazima atakuwa amechukia kupitiliza.
Lakini nakumbuka nilishawahi kufundishwa na mashoga zangu kuwa ukimkosea mwanaume kiwango cha mwisho akakupiga, basi kuna uwezekano kabisa akakusamehe kwa kosa ulilofanya tofauti na mwanaume ambaye kila siku anakupiga kwa kosa dogo, maana kama mwanaume huyo siku unamfanyia kosa kubwa utashangaa anakuacha bila kukugusa, lakini lazima akulime talaka tatu, au ndiyo nitolee hiyo hainaga msamaha.
Kwa hiyo wakati mume wangu alipokuwa akinipiga, nikawa naombea aendelee kunipiga tu kwa sababu kuna uwezekano akanisamehe. Lakini nikaona anaacha mara moja na kutulia kimya, akaanza kulia kama mtoto mdogo. Akaanza kunilaumu kwanini ninamsaliti wakati ananipenda na kunifanyia kila kitu.
Kitu kibaya ambacho wanaume wengi hawajui ni kwamba wenyewe ndiyo huwafanya wanawake wajue udhaifu wao na kuwatesa. Kwa mfano wakati mume wangu akinilaumu na kulia hovyo kama mtoto, tayari nilishajua udhaifu wake kuwa ananipenda na hawezi kuniacha hata kama ninaisaliti ndoa; na kama ningekuwa na roho mbaya basi ningeweza kumnyanyasa zaidi maana si nilijua hawezi kuniacha!
Mwanaume wa watu niliona analia mpaka nikamuonea huruma, nikaona ngoja nianza kumfunga kamba lakini lazima niwe makini maana nikichanganya maneno yangu lolote linaweza kutokea.
“mume wangu, naomba nisikilize kwanza,” nilisema kwa unyenyekevu huku nikiichukua ile simu na kuanza kuongea taratibu huku nikifungua meseji moja  hadi nyingine ili nijue jinsi ya kupanga uongo kufuatana na meseji hizo ili nisije nikajifungafunga.
“mimi kusema za ukweli, kuna mtu mmoja anakuwaga anatufundisha mambo mbalimbali ya mapenzi,”
“una maanisha nini?”
“ni masuala ya wapenzi jinsi wanavyotakiwa kuishi, kwenye ndoa yao,” nilisema huku nikijikuta naanza kubabaika maana sikuwa na uwezo wa kufunguka wazi kuwa eti tulikuwa tunafundishwa namna ya kuhondomora.   Nitaanzaje! Ingawa nilianza kuona kama vile maswali ya mume wangu yalikuwa yakinipeleka nielekee kufunguka ukweli huo.
“Kuwafunza masuala ya mapenzi sasa ndiyo mnakutana gesti na kufanya huo upumbavu?” alihamaki mume wangu.
“Jamani mume wangu, meseji haukuisoma vizuri, hii hapa hebu isome vizuri.”
Nilimpa simu nikitumia kipointi kimoja cha ile meseji kuchepusha kidogo ule ukweli, siyo kama nilidanganya lakini ni kusema uongo mweupe.

MESEJI ILISOMEKA HIVI;  
Mary : “ok tuache hayo vipi kesho utakuja na huyo mwanamke wako.”  
Mr X: “Yah nitakuja naye, itabidi nikuelekeze tutakapokutana. Lakini naye ameomba kuvaa maski usoni mwake anaona aibu kuangaliwa,” alisema Mr X.
Leo asubuhi:
Mary: “haya ndiyo naondoka hapa nije kwenye gesti gani, sitaki gesti za uswahilini.”
Mr X: “Njoo hapa Magomeni Makuti, kuna Lodge imejificha vizuri inaitwa Supaspoti, nipo chumba namba 23”
Mary: OK
**MWISHO WA MESEJI**

“Yaani siamini kama unanionesha nisome tena huo upuuzi wako!” alifoka kwa hasira mume wangu.
“hapana nakuonesha meseji hii,” nikamuonesha kwa kidole ile meseji kutoka kwa Mr X iliyosema;  “Yah nitakuja naye, itabidi nikuelekeze tutakapokutana. Lakini naye ameomba kuvaa maski usoni  mwake anaona aibu kuangaliwa.”
“ndiyo nini, unataka kuniambia huyo Mr X anawalala wote nyinyi wawili, bora hata huyo mwenzako hata ana aibu ya kujiziba uso, Mary Kweli!” alifoka tena mume wangu kiasi cha kuniogopesha kweli.
“Sio hivyo,  mbona tulikuwa na watu kibao akiwemo shoga yangu Blandina, Dr Ben na huyo Mr X ndiye aliyekuwa akitufundisha kwa vitendo, kwa hiyo tulienda kuonana naye gesti. Yeye alikuwa akituelekeza baadhi ya vitu kwa kumtumia huyo mwanamke anayemzungumzia amevaa maski kwa aibu ya kuangaliwa na watu wengi.
“Kama unabisha hebu chukua simu mpigie Blandina kama hauniamini,” nilijikuta nikisema kwa kujiamini na mimi baada ya kupata pointi ya kuitetea. Nilijua kwa vyovyote mume wangu alivyokuwa mtu wa heshima hataweza kumpigia simu Blandina na kumuuliza kuhusu suala hilo. Badala yake nikaona akiichukua ile simu na kuisoma tena na tena. 

ITAENDELEA IJUMAA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: