HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » SUMU YA PENZI SEHEMU YA THELASINI NA SITA (36)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Kesho yake asubuhi utaratibu ukawa uleule, baba hakutaka kabisa mimi na Jermaine tukae mbali naye, ndugu walizidi kuja na kunitazama kama nimegeuka picha ya maonesho, yaani hata yule ambaye alikuwa akinichukia alikuwa akiongea na mimi kwa heshima kweli.
Baadaye nilipata nafasi ya kukaa na marafiki zangu wa usichana hapo mtaani ambao wengi wao walikuwa wameshaolewa na kuzaa, hapo nikawa nakumbuka jinsi enzi zetu tulivyokuwa tukitawala mtaa mzima kwa uzuri wetu. 
Mimi, Catherine na Getrude lakini nakumbuka tulikuwa na rafiki yetu mwingine aliyeomba urafiki tena kwa kujipendekeza kweli, ambaye hakuwa mzuri wa sura kama sisi na hata hadhi yake haikuwa kama yetu sisi, alikuwa akiitwa Fatuma.
Fatuma japo kuwa alikuwa haendani kabisa na sisi, tulikuwa tukimtumia kutusaidia mambo yetu mengine hata kumtuma dukani na yeye alikuwa akifurahia na hata akiwepo hamna mtu anayeshughulika naye alikuwa kama vile haonekani. 
Marafiki kama hao wapo hasa kwenye vikundi vya wasichana, unakuta kuna yule msichana mzuri mno yeye ndiyo anakuwa kiongozi, halafu kuna wengine wanaoendana naye uzuri kidogo wanafatia chini yake na yule mbaya kabisa anakuwa ndiyo boya la kundi.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA  JUMANNE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: