Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, imetinga katika hatua robo fainali ya michuano ya Mataifa ya
Afrika baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Togo katika
kundi C.
Mfungaji anayeoongoza kufamania
nyavu katika michuano hiyo Junior Kabananga aliunganisha pasi ya
Chancel Mbemba na kufunga goli lake la tatu katika michezo mitatu.
Kabananga tena aligonga mwamba kwa
mpira wa kichwa kabla ya Ndombe Mubele kuongeza goli la pili kwa DR
Congo baada ya mapumziko.
Kodjo Fo-Doh Laba aliipatia
matumaini Togo baada ya kufunga goli, lakini mpira wa adhabu
uliopigwa na Paul-Jose M'Poku ulijaa wavuni na kuihakikishia ushindi
DR Congo.
No comments:
Post a Comment