Kiongozi wa muda mrefu wa Gambia,
Yahya Jammeh, amesema ataachia madaraka, hii ikiwa ni baada ya
kukataa kushindwa katika uchaguzi mkuu.
Akiongelea uamuzi wake huo kwenye TV
Jammeh, amesema kuwa hakuna umuhimu wa kumwagika hata tone la damu
katika nchi ya Gambia.
Kauli yake hiyo inafuatia mazungumzo
yaliyodumu kwa saa kadhaa baina ya Jammeh na wasuluhishi wa mataifa
ya Afrika ya Magharibi.
Jammeh ameiongoza nchi hiyo kwa
miaka 22 lakini alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka
jana na mpinzani wake Adama Barrow.
Barrow amekuwa katika taifa la
jirani la Senegal kwa siku kadhaa na aliapishwa kuwa rais wa Gambia
kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegal siku ya Alhamisi.





No comments:
Post a Comment