Mapacha wengi wanaozaliwa na wazazi wenye asili na rangi tofauti huwa na rangi moja, wengi huwa na hali ya uchotara. Lakini katika matukio machache kumetokea mapacha wenye kutofautiana kabisa rangi zao, mmoja anaweza kuwa mweupe na mwengine akawa na rangi nyeusi. Mapacha hao wanafahamika kama Biracial Twins au Mixed Twins.
Nini kinasababisha hali hiyo itokee? kwa kawaida mapacha wa kufanana hutungwa kwenye yai moja kabla halijagawanyika na kutengeneza watoto wawili wenye taarifa za kigenetiki zinazofanana. Lakini mapacha wenye rangi tofauti hutungwa katika mayai tofauti na kila yai linaweza kuchukua rangi ya mama au ya baba.
Uwezekano wa kupata mapacha wenye rangi tofauti ni 1 kati ya vizazi 500 vya mapacha wanaofanana.
Imeandaliwa na Moses Mutente
No comments:
Post a Comment