HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » » » MWANAMKE MMOJA AMEPOTEZA MAISHA KWA KUTOKWA NA DAMU NYINGI BAADA YA KUJIFUNGUA KWENYE DUKA LA DAWA WILAYANI MANYONI.

Mama moja wa kijiji cha Lulwangwa halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni amepoteza maisha kwa kutokwa na  damu nyingi  baada ya yeye na mume wake kuamua kwenda kujifungulia kwenye duka la dawa ambalo halikusajiliwa na aliyetoa huduma hiyo  hana ujuzi wa kuzalisha.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo  kaimu  mganga wa  halmashauri ya Itigi Daktari  Zuberi  Hamisi Abdalah amesema  pamoja na kwamba uchunguzi bado unaendelea ,lakini  mama   aliyefariki ametambulika kwa jina la  Helena Maduhu aliyekwenda kwenye duka la dawa kwa ajili ya kujifungua baada ya kuambiwa na muuguzi wa zahanati ya Itagata  aende hospitali ya Itigi baada ya wao kushindwa.
Akieleza mume wa marehemu  bwana bahame kanuda amesema yeye baada ya kuambiwa ampeleke mke wake katika hospita kubwa alikutana na bwana shingu hengwe ambaye ana duka la dawa na kumwomba kumsaidia kumzalisha mkewe .
Bwana Shingu Hengwe anayedaiwa kumzalisha mama huyo katika duka lake la dawa,baada ya  mzazi kufariki aliamua  kumsafirisha marehemu na pikipiki wakiwa na mumewake kumpeleka kijijini kwao, pikipiki ikaisha mafuta na yeye  alitoweka na kutafutwa zaidi ya saa nne kabla ya kukamatwa.
Mkurugenzi  wa halmashauri ya Itigi  ambaye  aliamua kusimamia shwala hilo  ilimlazimu kutuma watu  umbali wa zaidi ya kilomita kumina tano ambapo  marehemu alipo jifungulia kwenye duka la dawa na kukukuta mtoto aliyezaliwa   akiwa mzima kafungiwa  ndani  ya nyumba akilia huku wenye nyumba hawapo.

Chanzo: ITV Tanzania

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: