Idara ya Upelelezi nchini Marekani
imesema itafungua uchunguzi dhidi ya Madonna, baada ya mwanamuziki
huyo kusikika akiwaambia Wanawake walioandamana Jijini Washington
kwamba alifikiria kuilipua Ikulu kufuatia ushindi wa Donald Trump.
Katika maandamano hayo ya wanawake
kupinga sera za Trump, Madonna alitumia matamshi makali
yaliyolazimisha vyombo vilivyokuwa vikirusha mubashara tukio hilo
kuomba radhi mara kwa mara.
Akiongelea hasira alizokuwanazo
baada ya matokeo ya urais, Madonna aliwaambia waandamanaji alifikiria
mno kuilipua Ikulu, lakini alijua kuwa kufanya hivyo kusingebadilisha
chochote.
Waandamanaji wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali Jijini Washington DC
Theron mwenye hisia kali akitokwa na machozi wakati wa maandamano hayo
Mwanamuziki Alicia Keys naye alishiriki maandamano hayo ya Jijini Washington DC
Mwanamuziki John Legend naye alikuwa miongoni mwa waandamanaji waliounga mkono maandamano hayo ya wanawake
Muigizaji filamu mkongwe Whoopi Goldberg naye alikuwa ni miongoni mwa walioandamana Jijini Washington DC









No comments:
Post a Comment