HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » SUMU YA PENZI SEHEMU YA SITINI NA NANE (68)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kiukweli nilishangaa sana kumsikia baba naye akiweweseka kama mume wangu, nikawa nimechanganyikiwa kidogo, nikajiuliza  ina maana kumbe na baba naye alikuwa amerogwa na Fatuma kama mume wangu! He nilishangaa mno mimi nilijua wenzetu walituzidi ufundi wa mapenzi kumbe wanachanganya na mambo ya kilozi!
Basi mama hakujibu chochote, dada Mage ndiyo aliyesimulia kila kitu kilichotokea, wenyewe wakashangaa sana kusikia eti nilifungwa jela na mambo mengine ya ajabu waliyoyafanya.
“mke wangu tuondoke sasa hivi, lets go back to America I’m tired of this vodoo shit, I cant stay anymore,” aliongea mume wangu akionekana kuogopa kuendelea kubaki Tanzania, badala yake alitaka turudi Marekani haraka.
Hata mimi nikaona hiyo ni njia sahihi kwanza, lakini taratibu zote za kukata ticket na malipo ya ndege tukafanya haraka usiku huohuo kwa njia ya mtandao. Maana yake kesho kutwa mapema tusafiri. “Mama usihuzunike, tunaweza kufanya sherehe siku nyingine au tukawaalika mkaja kule Marekani, lakini hapa hali ilivyo siwezi kumfanya Mume wangu abakie,” nilimfariji mama nikiazimia kumuachia vita yake peke yake wakati mimi najaribu kuokoa ndoa yangu changa.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA JUMAMOSI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: