HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » WATU ZAIDI YA 60 WANUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA BASI NA GARI DOGO

 Watu wawili wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 60 wakinusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Ruksa Class kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Hilux katika eneo la Nhehelegani mkoani Shinyanga.
 Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Muliro Jumanne amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo (Jumanne) saa 3.00 asubuhi wakati basi hilo likitokea jijini Mwanza kuelekea mkoani Kigoma.
Kamanda Jumanne amewataja waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo kuwa ni Benard Bisansaba(45), ambaye ni mchumi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime na Kassim Shaaban (41) ambaye ni mwandisi wa halmashauri hiyo.
“Majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa matibabu,” amesema Jumanne. 
Picha zote na Masegwa Blog

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: