Kaishna wa Bima nchini Dkt .Boghayo Saqware akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima, mawakala wabima, wauza bima, jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.Picha na Vero Ignatus Blog.
Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya kaskazini Eliezer Rwekiza akizugumza katika uzinduzi huo wa uhakiki wa Bima kwa njia ya simu ya mkononi, uliofanyika Jijini Arusha leo, wa kwanza kulia ni Kamisha wa Bima Taifa Dkt.Boghayo Saqware,akifuatiwa na aliyepo kulia kwake ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Suleiman.
Meneja wa TEHEMA kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima
(TIRA) Aron Mlaki akiwa anawonyesha namna ya kutambua Bima kama ni
halali au ni feki kwa kutumia simu ya mkononi.
Mkurugenzi wa masoko kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) Bi.Adelaida Muganyizi akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima,mawakala wabima, wauza bima, jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.
Baadhi ya washiriki mbalimbali waliohudhuria kwenye
uzinduzi huo mfumo wa kuhakiki Bima kwa njia ya simu ya mkononi.
Afande James Manyama ambaye alimwalikisha kamanda
wa Polisi mkoa wa Arusha akizugumza katika uzinduzi huo.Piha na Vero
Ignatus Blog.
Mwanasheria wa Mamlaka ya usimamzi wa Bima (TIRA)
Arthur Mbena akiwa anawaelekeza wa kikosi cha usalama barabarani
namna ya kutambua Bima kama ni halali au feki kupitia simu ya mkononi
kwenye gari kama linavyoonekana pichani.
Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer
Rwekiza (aliyevaa koti suti nyeusi)akiwa anamuelekeza dereva wa gari
lililopo nyuma yao namna ya kutambua kama Bima iliyopo kwenye gari
lake ni halali,ambapo gari Ehilo lilikuwa na Bima halali.
Elimu ikiendelea kutolewa namna ya kutabua Bima
feki au halali kwa kutumia simu ya mkononi uliozinduliwa leo Jijini
Arusha na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA).
Meneja wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Usiamizi wa Bima
(TIRA)Aron Mlaki akitoa elimu kwa askari wa kikosi cha usalama
barabarani namna ya kutambua Bima feki au halali ,ni ya kampuni
gani, Bima gari la matumizi gani,aina gani ya bima kubwa au ndogo.Picha
na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Igantus.Arusha
Mamlaka ya
usimamizi wa Bima nchini(TIRA)imezindua mfumo wa uhakiki wa Bima kwanjia ya
simu za mkononi kanda ya Kaskazini ambapo zoezi hilo limeambatana na ukaguzi wa
bima kwenye vyombo vya moto na kubaini bima feki katika baadhi ya magari na
pikipiki.
Akizindua
mfumo huo kwa kanda ya kaskazini
uliofanyika jijini Arusha Kamishna wa Bima Nchini Dkt.Boghayo Saqware amesema
kuwa kampeni yao ina laengo la kuondoa bima feki sokoni ambazo
zinazouzwa ama kutengenezwa na wahalifu ,ambalo
kwa mujibu wa sheria wanafanya kosa la jinai.
“Tumeanzia
Pwani na sasa tupo Arusha na zoezi hili litakuwa endelevu,kwahiyo tunawaasa
wananchi wanunue bima halali,tumezindua mfumo ambao ni rahisi kwa mtu anaenunua
bima kujihakikishia kuwa bima hiyo ni feki au halali .”alisema
Dkt.Boghayo.
Kamishna
huyo amesema kuwa kwa miaka( 3) kesi (10) za Bima feki ziliamuliwa ,watu(5)
walihukumiwa kifungo jela,(2) wamelipa
bilioni 20,000,000, hadi 40,000,000,mashauri ya jinai yaliyopo
mahakamani yalifunguliwa mwaka 2016 Mbeya(1) Mafinga(2) Mara(1) na Dar es
salaam (3) na kufikia jumla ya kesi mpya 7,ambapo mashauri yaliyopo kwenye
uchunguzi wa polisi ni (10).
Kwa upande
upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya kaskazini Eliezer
Rwekiza amesema kuwa zoezi hilo katika Jiji la Arusha litaendelea kwa wiki
nzima ambapo wataelekea Kilimanjaro ,Tanga ambapo amesema kuwa
10% ya magari hapa nchini Tanzania hayana Bima
halali,amesema hadi sasa hapa nchini kuna makampuni 31 ya
Bima,mawakala 500 madalaliwa Bima ni zaidi ya
100.
“Kuna mtu
akienda kukata Bima anakuwa hajui kuwa hiyo ni feki,na kuna mwingine aknajua
kuwa hiyo ni feki na nashirikiana na yule anayemkatia,hivyo akibainika
anafutiwa leseni mkatajia halafu taratibu nyingine za kisheria zinafuata kwani
kwa utafiti ulikwisha kufanyika Jiji la Arusha ni la pili kwa kuongoza kwa pima
feki huku Jiji la Dar es salaam kinara”alisema
Rwekiza.I
Naye
meneja wa Tehama Aron Mlaki (TIRA)ameelezea namna ambavyo mtu
anaweza kuhakiki
Bima kwa njia ya simu ya mkononi ambapo amezitaja njia kuu mbili
ambazo ni inaweza
kuwa kwa intaneti au njia ya ujumbe mfupi wa
maneno.
“Kwa njia
ya inteneti (una sechi mis.tira.go.tz ,utaletewa mahali pa kujaza ,hakiki stika
kisha ukishahakiki stika inakuja ingiza namba za stika halafu bonyeza
hakiki,utaletewa maelezo ya bima yako kama ni halali au
feki,
Kwa njia
ya ujumbe mfupi (unaandika maneno stika unaweka namba ya
bima kwa
tarakimu zisizozidi 7 unatuma kwenye namba 15200 na hii ni kwa mitandao ya
Vodacom na Tigo peke yake.”
No comments:
Post a Comment