Timu ya Chelsea imeanza kuwauza
wachezaji wake ili kuwanunua Tiemoue Bakayoko na Alex Sandro, ambapo
sasa wamekuja na mbinu ya kuweka sharti la kuruhusiwa kuwanunua tena
wachezaji vijana inaowauza.
Tayari mchezaji wa Chelsea, Bertrand
Traore, amehamia Lyon ya Ufaransa kwa kitita cha paundi milioni 16
hapo jana, ambapo Chelsea itapata asilimia 15 ya faida iwapo Lyon
itaamua kumuuza baadaye.
Timu ya Chelsea pia imeweka kifungu
cha kumnunua tena itakapomuhitaji ili kuepusha kosa walilolifanya kwa
Romelu Lukaku, pia beki Nathan Ake anayewaniwa na Bournemouth kwa
kitita cha paundi milioni 20 amewekewa kifungu hicho.
Bertrand
Traore akiwa ameshatua rasmi katika timu ya Lyon
Chelsea ilimuuza Romelu Lukaku kwa Everton kwa kitita cha paundi milioni 28 bila kifungu cha kuweza kununua tena
No comments:
Post a Comment