Mkuu wa Wilaya yaMwanga, mkoani Kilimanjaro, Aaron Mbogho
Na Mwandishi Wetu
Wakazi wa Kijiji cha Ngulu kitongochi cha Mkongea wilaya ya Mwanga
wamesema kuwa tatizo la maji limekuwa tatizo sugu kwa muda mrefu bila
kutatuliwa hali inayosababisha ndoa nyingi kuvunjika. Mkazi wa kijiji hicho, Halima Miraji alisema kuwa tangu mwaka 2004
wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ambapo kwa
muda mrefu sasa maji yamekuwa yakitoka usiku wa manane tu.
Halima alisema kuwa mfumo wa maji ulijengwa kwenye kijiji jirani cha
Mgagani mwaka 1992 ambapo vijiji vyote viwili vilikuwa vikipata maji
kutokea hapo. Hata hivyo, alisema wakati wa mafuriko, miundombinu iliharibika na
hivyo kusababisha maji yapungue na ndipo viongozi wa vijiji hivyo
viwili walipoamua kuwa maji yawe yanafunguliwa kwenye kijiji cha Ngulu
nyakati ya mchana na kijiji cha Ngulu wakati wa usiku.
“Kutokana na changamoto hiyo, wanawake tunalazimika kuamka usiku wa
manane kuchota maji kwa kuwa kwa kawaida huwa yanakatika alfajiri,”
alisema Halima. Alisema kwa kuwa wanawake ndio wanaochota maji usiku na badhi ya
wanaume wachache ambao hawajaoa, kutokana na hilo alisema kuwa badhi
ya wanawake walijikuta wakiianza uhusiano na wanaume jambo ambalo
limefanya ndoa zao kuvunjika.
Alisema kila mtu hulazimika kuweka ndo moja kwenye foleni ya maji
iliyo na watu Zaidi ya hamsini kabla ya mzunguko kurudia mara ya pili,
tatu na kadhalika jambo ambalo liliwafanya badhi ya wanawake kuingia
kwenye vishawishi wakati wanasubiri kwenye foleni. Alisema kuwa changamoto nyingine, ni kuwa shughuli nyingi kama kilimo,
biashara na kutunza familia zimekuwa zikizorota kwa kuwa wanakuwa
wamechoka asubuhi baada ya kuchota bmaji usiku kucha.
Mkazi huyo aliyasema hayo wakati Kituo cha tafiti Twaweza ilipokuwa
kwenye zoezi la kujifunza hali halisi vijijini (immersion) ambapo
wafanyakazi wake wote waliweza kuishi kwa siku tatu na familia za
vijiji vya Ngulu kata ya Mwanga. Katika zoezi hili walibaini kuwa kukaa pamoja na jamii huwaleta karibu
na hivyo husaidia kueleza changamoto zao zinazowakabili kila siku
ambazo zimekuwa kikwazo cha maendeleo.
Kutokana na hilo, Twaweza waliweza kugundua changamoto nyingi,
ikiwemo, kwenye sekta ya afya, elimu, maji na kadhalika ambazo
zinahitaji ufumbuzi wa haraka. Kutokana na hilo wakazi wa Mwanga walishauri serikali kuhakikisha
inakuwa karibu na wananchi wake ikiwezekana kutenga muda wa kuishi
kwenye vijiji hivyo ilikuweza kutambua moja kwa moja kero zao na jinsi
ya kuzitatua.
Wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Twaweza, Aidan Eyakuze, wafanyakazi
wote wa Twaweza wakiwemo wale wa Tanzania, Kenya na Uganda walifunga
ofisi na kwenda kwenye vijiji mbali mbali vya mwanga kujifunza hali
halisi ya wakazi wa vijijini. Katika mwendelezo huo, mwenyekiti wa Kijiji cha Ngulu Modest Severine
alisema kuwa tatizo la maji limekuwa sugu katika kijiji hicho na kuwa
weka wakina mama katika wakati mgumu.
Alisema mradi wa maji ulipelekwa kwenye wnwo hilo mwaka 1992 lakini
kisima kilijengwa kwenye kijiji cha Mgagao kwa makubaliano kuwa maji
hayo yengetumika na wakati wa Mgagao pamoja na Ngulu. “Baada ya mradi kuharibiwa na mafuriko na badhi ya miundombinu kubebwa
na maji, viongozi walikubaliana kuwa wakazi wa Ngulu wafunguliwa maji
saa nane usiku,” alisema.
Alisema kuwa Mbunge wa jimbo hilo Bw Jumanne Maghembe alipewa tarifa
na kuahidi kutatua suala hilo. Alisema kwa mujibu wa mbunge huyo kuna mradi mkubwa wa maji unaoitwa
Maji ya Mungu uliokwenye hatua za awali ambao utakuwa unapeleka maji
kwenye vijiji vya Ngulu, Mgagao na Pangani.
Wakati huo huo, mjumbe wa serikali ya kijiji cha Ngulu, Kiende
Athumani nae alisema kuwa kitongoji cha Mkongea kimekuwa kikikabiliwa
na tatizo ya maji kwa muda mrefu. Alisema kutokana na changamoto za maji, wakazi wa …wamekuwa wakitumia
maji kumwagia mazao yao jambo ambalo linasababisha maji kutoka kidogo
nyakati za usiku.
Alisema kuwa serikali imetariwa kuwa kuna mradi wa maji ya Mungu
ambayo ikikamilika itakuwa ikitoa maji kwenye vitongaji mbali mbali
ikiwemo mkongea, Kavagala, Kivengere na Mabashara.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Aaron Mbogho alisema kuwa changamoto ya maji kwenye kijiji cha Ngulu unatafutiwa ufumbuzi.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Aaron Mbogho alisema kuwa changamoto ya maji kwenye kijiji cha Ngulu unatafutiwa ufumbuzi.
Alisema mradi wa Maji ya Mungu ukikamilika utakuwa unasambaza maji
kwenye wilaya ya Mwanga na Korogwe. “Wakandarasi wapo kwenye eneo la ujenzi, na tunategemea mradi awamu ya
kwanza uwe umekamilika ifikapo mwaka 2018,” alisema.
Alisema mradi awamu ya kwanza ukikamilika utakuwa umetatua kero ya
maji kwenye wilaya ya Mwanga na Same na hivyo kuhakikisha wakazi wa
Kijiji cha Ngulu wana maji ya kutosha. Aliongea kuwa, mradi awamu ya pili utanza pindi awamu ya kwanza
utakapokamilika na tatizo la maji litaisha au kupungua kwa kiasi
kikubwa.




No comments:
Post a Comment