HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » MAONESHO YA SABASABA 2017: MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA VIWANJA VYA SABASABA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akizugumza jambo wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi katika sekta ya Umma (Serikali), kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, wakati wa maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Anayemsikiliza na Meneja wa Usimamizi na Utawala wa Mifumo ya TEHAMA  wa PPRA, Bw.Bernard Ntelya.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akizungumza wakati akiwa kwenye banda la Mfuko huo

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akizungumza na Posta Masta Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Deo Kwiyukwa, wakati alipotembelea banda hilo.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
 Wafanyakazi hawa wakipatiwa maelezo mbalimbali yahusuyo huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam
 Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, (wapili kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), akizunguzma jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Elimu wa Mamlaka ya Udhibiti Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi. Saraha Kibonde Msika, ambaye alitembelea banda hilo. SSRA imeweka maafsia wake kila banda linalotoa huduma ya hifadhi ya jamii kwenye maonesho ya mwaka huu.
 Afisa wa WCF, (kulia), akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la WCF
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, (kushoto), akimsikilzia mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la Mfuko huo.


 Afisa wa WCF, Bi.Inocencia William, (kulia), akimpatia maelezo yenye kuhusu huduma za WCF mwananchi huyu aliyefika kujua nini hasa kazi ya Mfuko huo na faida zake kwa Mfanyakazi na Mwajiri
 Bw. Mshomba, (kulia), akiongongozana na Bi Laura, (kushoto) wakati akiwasuli kwenye banda hilo ili kuwahudumia wananchi. Kushoto ni Sebera Fulgence, Afisa Uhusiano mwandamizi wa Mfuko.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: