HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAISLAM WA AHMADIYYA KANDA YA ZIWA WAFANYIKA SHINYANGA

Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa (Ahmadiyya Muslim Jamaat Kanda ya ziwa) leo Jumapili Julai 9,2017 imefanya mkutano wa mwaka wa Jumuiya hiyo kwa mwaka 2017.

Mkutano huo umefanyika katika Msikiti wa Ahmadiyya Muslim Jamaat Tz Masjid Fath uliopo katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa huo.
Akizungumza wakati wa mkutano huo,Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alisema uislamu ni amani hivyo lengo la mkutano huo ni kuhamasisha amani katika jamii kwa kuwakumbusha waumini kumjua mwenyezi mungu.
Alisema endapo jamii itakuwa na hofu ya mungu itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza hata kumaliza kabisa vitendo viovu katika jamii ikwemo mauaji ya watu wasio na hatia kama vile vikongwe na watu wenye ualbino.
Katika hatua nyingine Sheikh Chaudhry alisema Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya ipo katika nchi 209 duniani ikiwemo Tanzania na mpaka sasa wamejenga misikiti 25 katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu.
“Jumuiya hii imeingia Tanzania takribani miaka minne iliyopita,kupitia mikutano yetu huwa tunaihamasisha jamii kuishi kwa amani,kufundisha watu watende mambo mema lakini pia tunaweka umeme wa jua na kuchimba visima katika vijiji ambavyo tumejenga misikiti yetu”,aliongeza.
Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame alisema sifa kuu ya uislam ni kuishi kwa amani na binadamu wengine na wala siyo kutisha watu wengine.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuendelea kuhamasisha amani katika jamii na kutoa mafunzo kwa waumini wao kama wanavyotamka na si vinginevyo.
“Viongozi wa dini mna jukumu la kuihamasisha jamii kuzuia makundi yasiyofaa katika jamii,toeni mafunzo yenye kujenga jamii na watanzania muwe tayari kutoa ushirikiano pale mnapoona kundi la watu flani wanataka kuleta uvunjifu wa amani”,alieleza Telack.
Aidha mkuu huyo wa mkoa aliipongeza Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kwa jitihada inazofanya katika kuhubiri amani katika jamii na kukemea vitendo viovu ikiwemo kuua watu wasio wakiwemo wazee na watu wenye ualbino pia kunyanyasa wanawake na watoto katika jamii.

MSIKILIZE HAPA CHINI KATIBU MSAIDIZI WA JUMUIYA YA WAISLAM WA AHMADIYYA TANZANIA,SHEIKH ABDULRAHMAN MOHAMMED AME AKIELEZA MAANA YA UISLAM

ANGALIA HAPA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO HUO
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (wa tatu kutoka kushoto) akimpokea mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (wa pili kushoto) kwa ajili ya kushiriki mkutano mkuu waJumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kanda ya ziwa mwaka 2017 uliofanyika katika Kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akitoa hotuba yake wakati wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kanda ya ziwa ambapo aliitaka jamii kuishi kwa amani.
Waumini wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya na wananchi wenye mapenzi mema wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo.
Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame akitafsiri kwa lugha ya Kiswahili hotuba ya Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry aliyokuwa anaitoa kwa lugha ya Kiingereza wakati wa mkutano huo katika kijiji cha Sungamile.
Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa, Waseem Ahmad Khan wakimsikiliza Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry.
Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame akitoa mada kuhusu Maana ya Uislamu.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa, Waseem Ahmad Khan akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba yake wakati wa kutano mkuu waJumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kanda ya ziwa mwaka 2017.
Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa eneo la tukio.Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akifuatiwa na Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo aliwasihi viongozi wa dini kuendelea kushirikiana serikali katika kudumisha amani ya nchi.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akimpa kipaza sauti Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa, Waseem Ahmad Khan wakati wa mkutano huo.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa, Waseem Ahmad Khan akizungumza wakati wa zoezi la kutoa zawadi ya vitabu vya dini kwa mgeni rasmi/mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu.Wa tatu kutoka kulia ni Kiongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Shinyanga Mwalimu Yusufu Gesonko.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akikabidhi mfuko uliobeba vitabu vya dini kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiwa ameshikilia kitabu kilichoandika "Mgogoro wa Dunia na Njia Kwenye Amani".
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Muliro Jumanne Muliro akipokea zawadi ya vitabu vya dini.Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia vitabu alivyopewa kama zawadi kutoka Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya. 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Muliro Jumanne Muliro akifurahia zawadi ya vitabu vya dini.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akisoma vitabu vya dini alivyopewa na Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya.
Waumini na wananchi wakiwa eneo la tukio.
Mbashiri/Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Morogoro Asif Butt akitoa mada kuhusu umuhimu wanawake na watoto katika familia na jamii kwa ujumla.
Akina mama wakiwa eneo la mkutano.
Viongozi mbalimbali wa serikali ya mkoa wa Shinyanga na viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa mkutano huo.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Tanga,Mohammed Bhati akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mwalimu Chande akisoma shairi
Mkutano unaendelea.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Dar es salaam,Khurram Shahzad akisoma Qur'an.
Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoa wa Dodoma,Khawaja Muzaffar  akisoma shairi.
Mkutano unaendelea.
Muonekano wa Msikiti wa Ahmadiyya Muslim Jamaat Tz Masjid Fath uliopo katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. 
Maneno yanayosomeka kwenye msikiti huo.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: